Habari

Usaili wa Maisha Plus kuanza Jumatatu


Usaili wa kusaka washiriki wa msimu mpya wa shindano la Maisha Plus unatarajia kuanza Jumatatu ijayo.
Tofauti na usaili wa mashindano yaliyopita, vijana hao 26 watatafutwa katika vijiji ambavyo Mama Shujaa wa chakula 15 walipatikana kutokana na mchakato uliofanywa na shirika la chakula na kilimo la Uingereza Oxfam ambalo msimu huu litashirikiana na waratibu wa shindano hilo.
Akiongea na TBC1 mtaribu wa mashindano hayo Masoud Kipanya amesema, “Vijana wa Maisha Plus wataingia kijijini, watakwenda kuchanganyika na hao kinamama, watakaa kwa siku tatu jumla kwa maana ya kwamba watakaa siku 12, 13 na siku 14. Katika hizi siku tatu vijana watakapochanganyika na hawa akinamama mle ndani tutatengeneza makundi ambapo kila mama mmoja mzalishaji wa chakula atakuwa na timu ya vijana tuseme watatu, wanne, sita kulingana na idadi ya washiriki wa Maisha Plus ambayo mwaka huu imeongezeka kutoka 18 hadi 26.”
Amesema washiriki hao wataingia kijijini mwezi October na mshindi wa mwaka huu atajinyakulia zawadi ya shiilingi milioni 20.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents