Burudani

Usahili wa Tusker Project Fame

Zaidi ya washiriki mia moja na thelathini wamejotokeza katika usaili wa kupata wawakilishio wa Tanzania jana katika shindano la Tusker Project Fame. Shindano hilo ambalo linafanyoka kwa mwaka wa nne linahusisha washiriki kutoka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo Sudani ya Kusini ambayo imeongzwa kuanzia mwaka huu.

Akizungumza na Bongo5 mchana leo katika hoteli ya Peacock ambako usahili huo umefanyika, Meneja wa habari na mawasiliano bibi Teddy Mapunda aliwaasa vijana wa kitanzania kuchangamkia fursa hiyo kwani ni moja ya sehemu itakayobadilisha maisha yao kwa kutumia kipaji cha muziki.

Teddy alisema kwamba shindano la mwaka huu ambalo ni la nne toka kuanzishwa kwake nchi washiriki zimeongezeka baada ya Sudan Kusini kuongezwa kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho mshindi wake atajinyakulia kitita cha Sh milioni 95 za Kitanzania pamoja na mkataba wa kurekodi albamu yake nchini Afrika Kusini katika studio za Gallo Records.

Shindano hilo la Tusker Project Fame linatarajiwa kuanza siku ya Jumamosi ya wiki ijayo na majibu ya walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania yatapatikana leo mchana baada ya majaji kuchuja washiriki watatu ambao ndio watatuwakilisha.

{youtube}HksRwX7qMo4{/youtube}

{youtube}Ww6JJ5o9PWA{/youtube}

{youtube}olh8oWbaOwc{/youtube}

{youtube}1MKtY2jznQQ{/youtube}

{youtube}J2lFcmIRtnA{/youtube}

{youtube}e1WTLR7xb_Y{/youtube}

{youtube}GAclgAevsXc{/youtube}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents