Michezo

Usain Bolt ameona isiwe tabu, bora kuwaachia wenye vipaji vyao, ameamua kutundika daluga kwenye mpira

Bingwa mara nane wa Olimpiki Usain Bolt ametangaza kuwa “maisha yake ya michezo yameisha”, baada ya kushindwa kuanza maisha rasmi ya soka la ushindani baada ya kung’ara kwenye riadha.

Kwa mujibu wa BBC, Bolt, raia wa Jamaica, 32, alikuwa akijinoa na kwa miezi miwili nchini Australia na klabu ya Central Coast Mariners, lakini akaondoka mwezi Novemba baada ya klabu hiyo kushindwa kupata fedha za kumsajili.

“Ilikuwa ni furaha kwa kadri ilivyodumu,” amsema Bolt ambaye bado anashikilia rekodi za dunia kwenye mbio fupi za mita 100 na 200. “Sitaki kusema kuwa hatukuliendea suala hili kama vile ilivyotakiwa, na naamini tulifanya kila ambacho tulitakiwa kufanya kwa namna sahihi.”


Usain Bolt alicheza kwa majaribio katika klabu ya Australia ya Central Coast Mariners, na kufunga goli katika mchezo wake wa kwanza

“Unaishi na unajifunza. Ulikuwa uzoefu mzuri kwangu – Nilifurahi kuwa kwenye timu.”

Mwezi Oktoba 2018, Bolt alifunga magoli mawili katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Macarthur South West, na akashangilia kama ada yake ya kujipinda kisha kunyoosha vidole viwili juu.

Timu hiyo ya Australi haikuwa ya pekee kutaka kumsaini Bolt – alikataa ofa ya klabu kutoka Malta iitwayo Valletta, sabau ikiripotiwa ni kushindwa kufikia kiwango cha mshahara alichokitaka.

Pia amefanya majaribio na klabu ya Stromsgodset kutoka Norway na miamba ya Ujerumani Borussia Dortmund.

Bolt, aling’atuka kwenye riadha mwaka 2017, amesema kwa sasa analenga kujikita zaidi kwenye masuala ya kibiashara. “Kwa sasa najielekeza kwenye biashara mbali mbali, kuna vitu vingi vinakuja, kwa hivyo najiingiza kwenye shughuli mbalimbali na kujaribu kuwa mfanyabiashara.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents