MichezoUncategorized

Usain Bolt kufanya majaribio ya soka Ujerumani

Usain Bolt amesema ameamua kufanya majaribio na klabu ya soka ya Ujerumani, Borussia Dortmund baada ya kustaafu mbio ya sprint.

Akiongea na Daily Express mchezaji huyo kutoka Jamaica mwenye rekodi ya dunia ya kukimbia kwa kasi zaidi katika mbio za mita 100 na 200 ni shabiki mkubwa wa Manchester United.

“Machi tutafanya majaribio na Dortmund na ndiyo itayoamua kama nitaweza kufanya kazi hiyo. Kama watasema mimi ninauwezo basi nitafanya mazoezi kidogo, na nitaanza kazi hiyo,” amesema Bolt.

“Inanifanya niwe na wasiwasi. Mimi siogopi lakini hii ni tofauti, hii ni soka sasa. Itachukua muda kurekebisha lakini mara baada ya kucheza mara chache nitazoea. Hii ni sawa na wakati nilivyoanza mbio. Nilikuwa na hofu kwa muda mpaka nilivyoanza kuzoeana na umati watu na kila mtu,” ameongeza.

Bolt mwenye miaka 31 alitangaza kustaafu mchezo wa riadha baada ya michuano ya dunia iliyofanyika mjini London mwezi Agosti 2017, pia alikiri kwamba moja ya ndoto zake kubwa ni kuweza kusaini Manchester United.

“Moja ya ndoto zangu kubwa ni kusaini kwa Manchester United. Kama Dortmund watasema niko vizuri, nitajifunza kwa bidii . Nimezungumza na Sir Alex Ferguson na nikamwambia nahitaji kuwa sehemu nzuri katika soka. Akaniambia kama nitafaa na kuwa tayari ataona kile anachoweza kufanya,” aliwahi kusema Usain Bolt wakati alipotangaza kustaafu riadha.

Kama majaribio yake yatafanikiwa, Bolt anaweza kutengeneza ushirikiano wa haraka na straika Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon endapo ataweza kumshawishi kocha wa timu hiyo Peter Stöger mwezi huo Machi.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents