Michezo

USAJILI: Chelsea yanufaika na Bertrand Traore

Aliye kuwa straika wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Burkina Faso, Bertrand Traore amejiunga na timu ya Lyon ya Ufaransa kwa dau la paundi milioni 8.8

Mchezaji Bertrand Traore 

Mchezaji huyo kinda mwenye umri wa miaka 21, ameingia mkataba wa miaka mitano wa kukitumikia kikosi hiko cha Ufaransa huku Chelsea ikitarajia kunufaika kwa asilimia 15 endapo Lyon itamuuza katika siku za usoni.

Traore aliiwezesha timu ya Ajax kuingia hatua ya fainali ya Europa League msimu uliyopita kabla ya kujiunga na Chelsea ambayo ameifungia jumla ya magoli manne katika michezo 16 aliyocheza.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents