Michezo

USAJILI: COSAFA yamtoa Abdi Banda asaini miaka mitatu Afrika Kusini

Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Simba, Abdi Hassan Banda amefikia makubaliano ya kuingia mkataba wa miaka mitatu na timu ya Baroka F.C ya Afrika Kusini .

Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Simba SC, Abdi Hassan Banda

Baada ya kufanya vyema katika michuano ya kombe la COSAFA Castle nchini Afrika Kusini akiiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tatu, mchezaji huyo wa Simba SC anatarajia kuanza maisha mapya katika timu hiyo ya Ga-Mphahlele, karibu na Polokwane, Limpopo ambayo inacheza Ligi Kuu ya nchini humo.

Banda anaondoka Simba SC aliyoichezea kwa miaka miwili, anajiunga na Baroka kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya KariaKoo.

Abdi Banda alikuwemo Banda kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza michuano ya COSAFA na kutwaa Medali ya Shaba baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Lesotho kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku wa jana Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg.

Kutoka na ushindi huo, Tanzania inaondoka na dola za Kimarekani 10,000 zaidi ya Sh. Milioni 22 kwa fedha za nyumbani, wakati Lesotho wamepata dola 8,300.

Mchezo wa Fainali ya COSAFA Castle 2017 unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng mjini Rusternburg baina ya Zambia dhidi ya majirani zao Zimbabwe wakati bingwa wa michuano hiyo akiondoka na dola 42,000 huku mshindi wa pili dola 21,000.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents