Michezo

USAJILI: Dirisha lijalo la usajili barani Ulaya

Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez  mwenye umri wa miaka 28, kunauwezekano mkubwa wa kujiunga na wapinzani wa Arsenal klabu ya Manchester City badala ya kwenda Real Madrid kama ambavyo wengi wanavyotarajia. (Daily Mirror).

Sanchez ni miongoni mwa washambuliaji waliorodheshwa na Real Madrid akiwemo mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 29, mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick Aubameyang mwenye umri wa miaka 28, mbali na mshambuliaji wa Torino, Andrea Balotti mwenye umri wa miaka 23, (Don Balon, via Sun)

Gharama iliyotumika kumsajili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazili, Neymar da Silva Santos Júnior  kutoka Barcelona kwenda PSG ya paundi milioni 222 iliyoweka rekodi ya dunia kinathamani ya paundi milioni 8 ya klabu yake ya zamani kulingana na rais wa klabu hiyo.(Esporte, via ESPN)

Mshambuliaji wa Tottenham, Vincent Janssen ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Fenerbahce hakukataa uhamisho wa West Brom kwa kuwa timu hiyo haikuwasilisha ombi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, (Birmingham Mail)

Klabu ya Real Madrid inajiandaa kuimarisha hamu yao ya kutaka kumsajili kipa wa Manchester United, David De Gea mwenye umri wa miaka 26, pamoja na kiungo wa kati wa Chelsea, Eden Hazard mwenye umri wa miaka 26, msimu ujao. (Don Balon, via Goal)

Klabu ya Real Madrid inatarajiwa kumsajili kinda Ricardo Rodrigues ,17, kutoka klabu ya Gremio Novorizontino katika kandarasi ya miaka 6 (AS, via Daily Star)

Liverpool itajaribu kumsajili beki wa Lazio Stefan de Vrij mwenye umri wa miaka 25, mnamo mwezi Januari (Calicomercato, via Talksport)

Mkufunzi wa klabu ya Leicester City, Craig Shakespeare anatumai kupokea habari za hatma ya kiungo wa kati Adrien Silva ,28, ambaye usajili wake kutoka Sporting Lisbon umekataliwa na Fifa. (Daily Mail)

Mchezaji anayelengwa na Liverpool Timo Werner, 21, ameiambia klabu ya RB Leipzig kwamba anataka kuchezea klabu kubwa msimu ujao .Mshambuliaji huo anasakwa na klabu ya Real Madrid. (Bild, via Yahoo)

Klabu ya Manchester United imekubali kumsajili kinda Charlie McCann kutoka klabu ya Coventry (Daily Mail)

PSG imemuongezea kandarasi kinda wa zamani wa Barcelona Kays Ruiz ,15, kwa kandarasi ya chipukizi ya hadi 2020 (ESPN)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents