Michezo

USAJILI: Dirisha lijalo la usajili barani Ulaya

Tottenham wanapanga kumsajili mshambuliaji wa Besikitas, Cenk Tosun wakati wa dirisha la usajili la mwezi Januari ambaye alizitolea nje timu za Crystal Palace na Newcastle msimu uliopita. (Talksport)

Mchezaji wa Besikitas, Cenk Tosun

Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania ilishindwa kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezman  mwenye umri wa miaka 26, kwa dau la paundi milioni 124, msimu uliopita huku Manchester United pia walikuwa wakionyesha niya ya kuinasa saini  ya mchezaji huyo wa Ufaransa. (Mundo Deportivo via Talksport)

Manchester United wanamtaka mshambuliaji wa Genoa, Pietro Pellegri ambaye alifunga mara mbili dhidi ya lazio siku ya Jumapili. (Gazzetta dello Sport via Metro)

Manchester United na Manchester City ni miongoni mwa klabu ambazo zinapanga kumsajili mshambuliaji wa Lazio, Sergej Milininkovic-Savic, 22 (Daily Mirror)

Mshambuliaji wa Arsenal, Jack Wilshere mwenye umri wa miaka 25, anahitaji kuhamia West Ham dirisha la mwezi Januari kwa kuwa Arsenal haijaanza mazungumzo yoyote ya kumpatia kandarasi mpya(Daily Star)

Real Madrid wanataka kumuuza mshambuliaji Karim Benzema, 29, kwa Arsenal. (Don Balon via Daily Star)

Manchester City wamekuwa wakitumia ushawishi wa kiungo wa kati wa Brazili ili kusaidia kupata wachezaji wanaowataka (Manchester Evening News).

Kiungo wa kati wa Manchester United, Paul Pogba amewatambua Michael Carrick na Paul Scholes kama wachezaji wawili waliokuwa na athari kubwa katika mchezo wake katika uwanja wa Old Trafford (Daily Mirror)

Wayne Rooney bado atapewa fursa ya kuwa balozi wa Manchester United licha ya kukiri kunywa na kuendesha gari (Daily Star)

Wachezaji wa Barcelona walionyesha kumuunga mkono Ousmane Dembele, ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti kwa kuvaa shati iliokuwa na ujumbe Courage Ousmane kabla ya mechi yao dhidi ya Eiber(Daily Mirror)

Mshambuliaji wa Manchester City, Gabriel Jesus anatarajiwa kuandikisha kandarasi mpya na kilabu hiyo akitarajiwa kupata nyongeza maradufu ya kipato cha paundi150,000 kwa wiki. (Daily Mirror)

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 28. Mchezaji huyo wa Chile pia anasakwa na Manchester City. (Sun)

Chelsea inachunguzwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani ‘FIFA’ kwa kukiuka sheria zinazowalinda wachezaji wenye umri mdogo.

Klabu hiyo inasema inakubaliana na sheria zote za FIFA wakati inapowateua wachezaji wake (Daily Mail)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents