Michezo

USAJILI: Hatukuondoka Azam FC kwa kulipiza kisasi- Aishi Manula

Kufuatia kuhusishwa na heka heka za usajili kwa goli kipa bora wa msimu uliomalizika, Aishi Salum Manula kujiunga na klabu ya Simba SC kwaajili ya kuitumikia katika msimu ujao wa ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa.

Golikipa wa Azam FC na timu ya Taifa ya Tanzania, Aishi Manula

Mchezaji huyo amezungumzia mahusiano yake na matajiri wa Dar es salaam, klabu ya Azam FC toka alipoamua kuachana nayo kwaajili ya Msimu wa ligi wa 2017/18.

“Nimeweza kulelewa pale na kuishi pale kwa takribani miaka sita so nimeyafurahia maisha ambayo nimeishi kipindi chote nilipokuwa pale Azam FC,  ni maisha ambayo nitayamisi huko ambako ninapoenda  kwa sababu Azam ni kama nyumbani.

“kama ingekuwa tunalipa kisasi ungeona basi hata Azam wanazungumza vibaya kuhusiana na sisi nimepata taarifa Nassor Idrissa alizungumza na alitutakia kila  lakheri huko tunapoenda na sio tumeondoka pale kwa kulipa kisasi”.

Mlindamlango huyo wa Azam FC na Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, ameyasema hayo kupitia kipindi cha Mshikemshike Viwanjani kinachorushwa na Azam TV.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents