Michezo

USAJILI: Kylian Mbappe atua PSG kwa vipimo

Mshambuliaji kinda wa Klabu ya AS Monaco, Kylian Mbappe anatarajiwa kukamilisha usajili wake wa mkopo na kwenda kwa matajiri wa Ufaransa timu ya Paris Saint-Germain (PSG).


Mchezaji huyo anatarajiwa kutua nchini Ufaransa siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Ufaransa.

Kituo cha redio cha Ufaransa siku ya Jumapili kiliripoti kuwa PSG wamekubali kulipa Euro milioni 180 ambazo sawa na dola za marekani 215,000,000 ikiwa ni pamoja na mafao kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 18.

Usajili huo utaweka historia katika uhamisho kuwa usajili wa pili wa gharama kubwa zaidi katika soka baada ya Neymar, ambaye alijiunga na PSG kutoka Barcelona kwa Euro milioni 222 mapema mwezi huu.

Hata hivyo kuna wasiwasi zaidi kuhusiana na kile kilicho juu ya mkutano wa UEFA wa Fedha unaohusu gharama kubwa katika usajili wa wachezaji Fair Play (FFP) na ndio maana PSG wanataka kwanza kumsajili kwa mkopo Mbappe .

Monaco na PSG siku ya Jumapili zilifikia makubaliano ya Kylian Mbappe kwenda PSG kwa gharama ya usajili wa Euro milioni 180.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents