Michezo

USAJILI: Mashabiki wa Yanga SC wachoma jezi ya Niyonzima (Video)

Kuondoka kwa mchezaji Haruna Niyonzima ndani ya klabu ya Yanga SC, kumeonyesha kuwaumiza mashabiki wa klabu hiyo ambapo moja kati ya kundi la mashabiki wameamua kuchoma jezi ya mchezaji huyo.

Mashabiki wakionekana kuichoma moto jezi yenye jina la Niyonzima na namba 8 mgongoni namba ambayo hutumia mchezaji huyo uwanjani

Hapo jana Klabu ya soka ya Yanga ilitoa taarifa ya kuachana na aliyekuwa mchezaji wake wa kimataifa raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima baada ya kushindwa kuafikiana.

kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa alisema Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hawataweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kutokana na kushindwa kkuafikiana katika mazungumzo.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents