USAJILI: Shaaban Iddi Chilunda atambulishwa rasmi Hispania

Mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Iddi Chilunda ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa klabu ya CD Tenerife kutoka nchini Hispania.

Chilunda ambaye alikuwa akiitumikia Azam FC amesajiliwa na klabu hiyo ya CD Tenerife inayoshiriki Segunda Division (ligi daraja la kwanza) kwa mkataba wa miaka miwili.

Kinda huyo aliyezaliwa Julai 20 mwaka 1998 anakumbukwa zaidi baada ya siku za hivi karibuni kutupia jumla ya mabao manne peke yake kwenye mchezo wa  Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda na kuweka rekodi kwenye soka la Afrika Mashariki.

📷 Shaban Idd Chilunda tayari ni mchezaji wa . kuanzia majira ya saa 13:00 atakwnda kufanyiwa vipimo vya afya . 🇹🇿.

Shaaban Iddi Chilunda ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Tenerife kutoka Azam baada ya klabu hiyo kumsajili Farid Musa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW