Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania huenda wakaamua kumgeukia, Mesut Ozil mwenye umri wa miaka 28, iwapo watashindwa kumpata kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho.

Tokeo la picha la Mesut Ozil

Mchezaji wa Arsenal, Mesut Ozil 

Huku hatma ya Neymar kwenda PSG ikiwa inazungumzwa, Barca wanatafuta mchezaji wa kuziba pengo lake. (Don Balon)

Arsenal na Tottenham wamepeleka maskauti wao kumtazama mshambuliaji kinda wa Caen, Yann Karamoh, ambaye ametajwa kuwa kama “Kylian Mbappe mwingine”. Chipukizi huyo anafuatiliwa pia na Forentina na AC Milan na Inter Milan. (Sunday Mirror)

Mshambuliaji kinda wa Caen, Yann Karamoh

Beki wa kulia wa matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain, Serge Aurier amekubali kujiunga na Manchester United, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ameruhusiwa kuondoka na meneja Unai Emery. (Sky Sports)
Alexis Sanchez anafikiria kuwasilisha ombi la kuondoka Emirates ili kulazimisha uhamisho wake kwenda Manchester City. Sanchez anataka sana kuondoka, na Pep Guardiola yuko tayari kufanikisha usajili wake. Sanchez anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, na Arsenal wako tayari kutoa 300,000. (Daily Mirror)

Tokeo la picha la Alexis Sanchez

Mchezaji wa Arsenal, Alexis Sanchez

Southampton wana matumaini kuwa Virgil van Dijk atabadili mawazo na kurejea mazoezini na kikosi cha kwanza wiki hii. Southampton hawataki kumuuza beki huyo anayenyatiwa na Liverpool. (Daily Echo)

Cristiano Ronaldo hataki Real Madrid imnunue, Kylian Mbappe kwa sababu huenda kinda huyo ‘akamfunika’ na kuathiri nafasi ya kushinda Ballon d’Or. (Diario Gol)

Tokeo la picha la Kylian Mbappe

Mchezaji wa  AS Monaco, Kylian Mbappe

Matumaini ya Liverpool kumsajili Naby Keita yanazidi kupata wakati mgumu baada ya Inter Milan nayo kuingia katika harakati za kumtaka kiungo huyo. (CalcioMercato)

Chelsea wanapanga kutaka kumchukua kinda wa Celtic, Karamoko Dembele, 14. (The Sun)

Kiungo wa Everton, Ross Barkley atalazimika kupunguza mshahara anaotaka iwapo anataka kujiunga na Tottenham ambao wapo tayari kumlipa pauni 120,000 kwa wiki, sawa na ambazo amezikataa Everton. (Mirror)

Ross Barkley

Kiungo wa Everton, Ross Barkley

Everton watashikilia bei ya pauni milioni 35 kumuuza Ross Barkley licha ya kuwa mkataba wake utamalizika baada ya mwaka mmoja. (Mail)
Barcelona watawashitaki PSG kwa UEFA kwa kukiuka kifungu cha fedha hata kama hawatolipa pauni milioni 197 za kutengua kifungu cha uhamisho cha Neymar. (El Larguero)

PSG wana uhakika wa kumsajili Neymar, na tayari wanapanga jinsi ya kumtambulisha mchezaji huyo kwa mashabiki. (ESPN)
West Brom wanamtaka beki wa zamani wa Arsenal, Thomas Vermaelen, 31, ambaye alihamia Barcelona miaka mitatu iliyopita. (Sky Sports)

Tokeo la picha la Neymar

Mchezaji wa Barcelona, Neymar

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema wachezaji kama Alexis Sanchez na Mesut Ozil ambao wanaingia katika mwaka wa mwisho wa mikataba yao ndio “wazuri zaidi” kwa sababu watataka kuonesha kiwango cha juu. (Sun)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho hana mpango wa kumtoa kwa mkopo kiungo Andreas Pereira, 21, baada ya mchezaji huyo kuonesha kiwango katika mechi za kujipima nguvu. (Sun)

Meneja wa Bacelona, Ernesto Valverde anataka kumpa namba Thomas Vermaelen msimu huu baada ya kufurahishwa na kiwango alichoonesha kwenye mechi za kujipima nguvu. (AS)

Tokeo la picha la Thomas Vermaelen

Mchezaji, Thomas Vermaelen

Wachezaji wa Manchester City wanazungumzia waziwazi kuwasili kwa Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwa mkataba wa pauni milioni 50. (Manchester Evening News)

By Hamza Fumo

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW