Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Wakili wa Diego Costa ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Chelsea baada ya klabu hiyo kupinga Costa kwenda AC Milan kwa mkopo kabla ya kwenda Atletico Madrid mwezi Januari. (Mirror)


Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Edin Hazard mwenye umri wa miaka 26, amewasiliana na Barcelona kuhusu kwenda kuziba pengo la Neymar. (Don Balon)

Chelsea wapo tayari kupambana na Liverpool katika kutaka kumsajili beki wa kati wa Southampton, Virjil van Dijk mwenye umri wa miaka 26, kwa kutoa pauni milioni 50. (The Times)

Kiungo mshambuliaji wa PSG, Javier Pastore, amempa Neymar namba yake ya jezi – 10- akisema “anataka ajisikie yuko nyumbani”. (Tovuti ya PSG)

Meneja wa Real Madrid anaamini kuwa klabu yake lazima imuuze, Gareth Bale mwenye umri wa miaka 28, ikiwa inahitaji kumsajili kinda wa AS Monaco, Kylian Mbappe mwenye umri wa mika 18, (Marca)

Manchester United wanafuatilia kwa makini hali ilivyo Real Madrid na huenda wakapanda dau la pauni milioni 90 kumtaka Gareth Bale, 28. (Daily Star)

Tokeo la picha la Gareth Bale

Jose Mourinho anaamini anaweza kumsajili Gareth Bale kwa chini ya pauni milioni 90. (Don Balon)
Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa mwenye umri wa miaka 28, atawasilisha maombi rasmi ya kutaka kuondoka Stamfrod Bridge. (Independent)

Beki wa Southampton, Virgil van Dijk mwenye umri wa miakaa 26, huenda akakosa mechi za mwanzo za msimu kutokana na hatma yake kutofahamika. (Telegraph)

Jurgen Klopp amekuwa na mawasiliano ya karibu na Kylian Mbappe18, huku Liverpool wakiendelea kumfuatilia mshambuliaji huyo wa Monaco. (L’Equipe)

Tokeo la picha la Kylian Mbappe

Meneja wa Everton, Ronald Koeman bado ana matumaini ya kusajili mshambuliaji mwingine, huku bado wakiendelea kumtaka Olivier Giroud, 30, wa Arsenal. (Liverpool Echo)

Kiungo wa Bayern Munich Arturo Vidal anataka kurejea Italy, baada ya kufikia makubaliano na Inter Milan. (FCInterNews)

Meneja wa Crystal, Palace Frank de Boer anataka kumsajili beki wa Manchester United, Timothy Fosu-Mensah, 19. (Sun)

Anderlecht ya Ubelgiji wameingia katika mbio za kumsajili beki wa zamani wa Arsenal, Thomas Vermaelen 31, ambaye pia anasakwa na West Brom. (Birmingham Mail)

Tokeo la picha la Arsenal, Thomas Vermaelen

Mabingwa wa Ufaransa, Monaco, wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 45 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 28. (Sun)
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, alibusu nembo ya Arsenal mbele ya waandishi wa habari wakati wa mazoezi siku ya Alhamisi. (Telegraph)

Dau la Arsenal kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, limekataliwa. (Mundo Deportivo)
Borussia Dortmund wapo tayari kuzungumzia uhamisho wa Ousmane Dembele, 20, kwenda Barcelona, ikiwa tu Barca watakuwa tayari kutoa euro milioni 100. (Bild)

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents