Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp ndiyo kizingiti kikuu katika majadiliano yoyote kuhusu usajili wa mchezaji wake, Philippe Coutinho. (Marca)

Philippe Coutinho hatowasilisha maombi ya kutaka kuondoka Liverpool ili kulazimisha uhamisho wake. (Sport)

West Ham wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 25 kumtaka kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho mwenye umri wa miaka 25. (Daily Mail)

Kiungo wa Chelsea, Willian mwenye umri wa miaka 29, alizungumza na Manchester United msimu huu kuhusu uwezekano wa kuhamia Old Trafford. (Goal)

Tokeo la picha la Chelsea, Willian

Tottenham wapo tayari kutoa pauni milioni 55 kumsajili beki wa Ajax, Davinson Sanchez. (The Sun)
Paris Saint-Germain wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 18, kwa pauni milioni 163, na tayari wamekamilisha mkataba na Fabinho, 23, pia wa Monaco. (Daily Record)

Iwapo Kylian Mbappe ataondoka, Monaco wataamua kumfuatilia mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Carlos Bacca anayeichezea AC Milan. (Caracol Radio)

Tokeo la picha la Kylian Mbappe
Chelsea wamepanda dau la pauni milioni 35 kumtaka kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Daily Star)
Chelsea wanazidi kuonekana kuwa na nafasi zaidi ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Everton Ross Barlkey, ambaye pia ananyatiwa na Tottenham. (Daily Telegraph)

Arsenal wana wasiwasi kuwa mshambuliaji wake Alexis Sanchez, 28, huenda akataka kulazimisha uhamisho wake kuondoka Emirates. (Daily Mirror)
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anataka kusajili angalau mchezaji mmoja zaidi kabla ya dirisha la usajili kufungwa huku beki wa kushoto, Danny Rose, 27, na winga wa Inter Milan Ivan Perisic wakiendelea kunyatiwa na United. (Manchester Evening News)

Tokeo la picha la Danny Rose

Jose Mourinho ameitaka Manchester United kupanda dau la pauni milioni 100 kumtaka Gareth Bale wa Real Madrid. (The Sun)
Danny Rose amesema hana mpango wa kuondoka Tottenham, lakini anaamini anastahili kulipwa zaidi kuliko anavyolipwa sasa. (Sun)
Danny Rose ameitaka Tottenham kusajili wachezaji wenye majina makubwa. (Sun)

Barcelona watarejea tena Liverpool na dau la nne la kumtaka kiungo mshambuliaji kutoka Brazil Philippe Coutinho, 25. (Daily Mail)
Barcelona na Atletico Madrid wanapambana katika kutaka kumsajili Lautaro Martinez anayechezea Racing Club ya Argentina. (El Grafico)

Barcelona wameambiwa walipe pauni milioni 135 kama wanataka kumsajili Ousmane Dembele, 20, wa Borussia Dortmund. (the Guardian)

Newcastle wamefanikisha usajili wa mkopo wa winga wa Chelsea, Kenedy, 21. (Daily Mirror)
Manchester United wameanza mazungumzo na Zlatan Ibrahimovic, 35, kuhusu mkataba mpya, wakati mchezaji huyo akiendelea kupata nafuu ya jeraha lake la goti. (Daily Mail)

Zlatan Ibrahimovic anaendelea na mazoezi na amemuambia Jose Mourinho kuwa anataka kubakia Old Trafford. (Guardian)

Meneja wa Marseille Rudi Garcia amesema mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, “atawafaa sana” lakini mfaransa huyo hana mpamgo wa kujiunga na klabu hiyo ya Ligue 1. (L’Equipe)

Meneja wa Newcastle, Rafael Benitez amezungumza na Arsene Wenger wa Arsenal kuhusu kutaka kumsajili, Lucas Perez, 28, lakini Arsenal wameshikilia bei ya pauni milioni 13.4. (Chronicle)

Tokeo la picha la Lucas Perez

Kiungo wa Real Madrid, Isco, 25, anakaribia kusaini mkataba mpya na hivyo kuwanyima nafasi Manchester United na Arsenal ya kumsajili. (Independent)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte ameiambia bodi ya klabu yake kumsajili beki wa kulia wa Barcelona Sergi Roberto, 25. (Sport)
Beki wa Valencia Joao Cancelo mwenye umri wa miaka 23, anakaribia kujiunga na Chelsea. (Don Balon)

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents