Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Baba mzazi wa mchezaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi  mzee Jorge Messi amezungumza na uongozi wa juu wa klabu ya Manchester City kuhusiana na hatima ya mtotowake kujiumga na timu hiyo.

Na huko nchini Ufaransa kinda wa AS Monaco, Kylian Mbappe anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na PSG kwa dau la Euro milioni 150. Monaco na PSG tayari zimefikia makubaliano ingawa wanasubiri kuona nani kati ya Julian Draxler, Lucas Moura au Javier Pastore atakuwa tayari kwenda Monaco kama sehemu ya mkataba huo. (L’Equipe)

Beki wa West Brom Jonny Evans mwenye umri wa miaka 29, anatarajia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 30 kwenda Manchester City wiki ijayo. (Mirror).

Manchester City hawajakata tamaa ya kumsajili mchezaji wa Arsenal, Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 28, na wanafikiria kupanda dau la pauni milioni 50, kumsajili mchezaji huyo kabla dirisha la usajili halijafungwa wiki ijayo. (Times).

Image result for Arsenal, Alexis Sanchez

Manchester City wanataka kupanda dau la Euro milioni 40 kumsajili beki wa Espanyol, Aaron Martin mwenye umri wa miaka 20 (Sport)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amezuia uhamisho wa mkopo wa kiungo, Andreas Pereira kwenda Valencia. (Marca)

Barcelona wanajiandaa kupanda dau kumchukua winga wa klabu ya Chelsea, Willian mwenye umri wa miaka 29. (Times)

Image result for Chelsea, Willian

Chelsea wamepanda dau jipya la pauni milioni 35 kumtaka winga wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain mwenye umri wa miaka 24. (Telegraph).

Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 32 kumsajili kiungo wa Leicester City, Danny Drinkwater mwenye umri wa miaka 27. (Sun)

Nyota wa Chelsea, Eden Hazard atafanya kila awezalo kulazimisha uhamisho wake kwenda Real Madrid msimu huu. (Don Balon)

Barcelona wamekuwa na mazungumzo na PSV Eindhoven kuhusiana na uhamisho wa winga kinda Steven Bergwijn, 19. (gianlucadimarzio.com)

Schalke wamewaambia Barcelona wanaweza kumsajili Leon Goretzka, ili kuzuia mahasimu wao Bayern Munich wasimchukue. (Mundo Deportivo)

Vincent Janssen na Kevin Wimmer wa Tottenham wanakaribia kuhamia West Brom. (Sun)

Beki wa Manchester City Eliaquim Mangala anakaribia kuhamia Inter Milan. (Sky Sports)

Paris Saint-Germain wanafikiria kumsajili kipa wa Napoli Pepe Reina, 34. (AS)

Barcelona wanakaribia kukamilisha usajili wa Angel Di Maria, 29, kutoka PSG. (Sport)

Tottenham wanajiandaa kupanda dau jipya kumtaka mshambuliaji wa Lazio Balde Diao, 22, ambaye pia amehusishwa na kwenda Juventus. (Corriere dello Sport)

Tottenham wapo kwenye mazungumzo ya kina na PSG kuhusu uhamisho wa beki Serge Aurier kwa pauni milioni 24. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell, 25, ameiambia klabu yake kuwa hataki kwenda popote kwa mkopo msimu huu. (Guardian)

Arsenal watakubali pauni milioni 14 kutoka kwa Deportivo La Coruna ili kumsajili Lucas Perez kabla ya dirisha la usajili kufungwa wiki ijayo. (Evening Standard)

Beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk amekutana na Chelsea bila ruhusa ya klabu yake. (Star)

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, huenda akaondoka Hispania kabla ya mwisho wa wiki hii. (El Pais)

Kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho mwenye umri wa miaka 25, anafikiria kutoa taarifa rasmi kwa umma kuzungumzia kutoridhishwa kwake na klabu hiyo, ili kulazimisha uhamisho wake. (Yahoo Sports)

Juventus wanapanga kupambana na Liverpool katika kumsajili beki wa Schalke Benedikt Howedes. (Bild)

Inter Milan wamepanda dau la kumtaka beki wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25, kwa mkopo, katika mkataba wa kumsajili kikamilifu baadaye kwa pauni milioni 20. (Mirror)

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents