Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 30 wa kiungo wa Leicester City, Danny Drinkwater mwenye umri wa miaka 27, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Daily Telegraph)

Manchester City wapo tayari kuwapa Arsenal pauni milioni 70 pamoja na beki, Jason Denayer ili kumsajili, Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 28. (Daily Star)

 

Manchester City wanajiandaa kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick Aubameyang iwapo watashindwa kumsajili Alexis Sanchez. (Le10Sport)

Leicester City wamepanda dau la pauni milioni 23, kutaka kumsajili beki wa West Brom, Jonny Evans mwenye umri wa miaka 29. (BBC)

Hatma ya meneja wa Crystal Palace iko mashakani baada ya kupoteza mechi tatu za EPL. (Guardian)

Meneja wa West Ham, Slaven Bilic anapambana vikali kulinda kazi yake baada ya kupoteza mechi tatu za mwanzo za EPL. (Sun)

Liverpool wamemuulizia kiungo wa Monaco, Thomas Lemar mwenye umri wa miaka 21, na wapo tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ya klabu kwa kutoa pauni milioni 55. (Daily Telegraph)

Paris Saint-Germain wamefikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 18, na kuweza kukamilisha usajili wa pauni milioni 166 msimu ujao. (L’Equipe)

Manchester United wamewapa Real Madrid pauni milioni 92 kutaka kumsajili Gareth Bale. (Daily Star)

Barcelona wanamuona Marcus Rashford wa Manchester United kama mrithi wa baadaye wa Luis Suarez. (Don Balon)

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema yuko tayari kumruhusu Divock Origi, 22, kuondoka kwa mkopo iwapo klabu yake itaongeza wachezaji wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Liverpool Echo)

 

Beki wa Arsenal, Shkodran Mustafi mwenye umri wa miaka 25, anajiandaa kuondoka Emirates na kwenda Inter Milan, mwaka mmoja tu baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 35 kutoka Valencia. (ESPN)

West Brom wamepanda dau la pauni milioni 10 kumtaka kiungo wa Fenerbahce Josef de Souza, 28, na pia wamemuulizia beki wa Bournemouth Tyrone Mings, 24. (Daily Mail)

Swansea watapanda dau la pauni milioni 13 kutaka kumsajili tena mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony, aliouzwa kwenda City kutoka Swansea mwaka 2015 kwa pauni milioni 28. (Daily Mail)

Inter Milan wanakaribia kumsajili Keita Balde wa Lazio kwa pauni milioni 27. (Daily Mirror)

Birmingham City wanazungumza na kiungo wa kimataifa wa Ghana Afiriye Acquah, 25, kutaka kumsajili kutoka Torino. (Sky Sports)

Stoke City wamefikia makubaliano na Tottenham ya kumsajili beki Kevin Wimmer mwenye umri wa miaka 24, kwa pauni milioni 15. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy mwenye umri wa miaka 30, ananyatiwa na Las Palmas ya Uhispania na Calgiari ya Italia. (Daily Mail)

Meneja wa Chelsea atabakia Stamford Bridge hata kama watashindwa kuongeza wachezaji wengine wapya. (Evening Standard)

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente mwenye umri wa miaka 32, wakilenga kusajili wachezaji watatu wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)

Kipa wa Liverpool Simon Mignolet mwenye umria wa miaka 29, ananyatiwa na Napoli. (Gianluca Di Marzio)

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents