Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, huenda akahamia Liverpool kwa pauni milioni 60 msimu huu. Mchezaji huyo amesisitiza anahitaji kwenda Liverpool. (Sun)

Beki wa Southampton Virgil van Dijk

Arsenal wanafikiria kutoa pauni milioni 45 kumchukua beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Express)

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amepigwa picha kwenye Instagram akiwa amevaa jezi ya Atletico Marid na kuandika “mpe salaam zangu Conte”. (Mail)


Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, baada ya kumkosa Romelu Lukaku, 24. (Sky)
Chelsea wameonywa na Borussia Dortmund kuwa wana wiki moja tu ya kumsajili Pierre Emerick-Aubameyang. (The Sun)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anadhani kuwa ataweza kumshawishi Alexis Sanchez, kutoondoka Emirates. (Mirror)
Vinginevyo Arsene Wenger anafikikia kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele, 20. (Star)
Arsene Wenger amekata tama ya kumsajili Kylian Mbappe, 18, na badala yake sasa anaelekeza nguvu katika kumsajili Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco. (Telegraph)


Mchezaji wa klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa, Kylian Mbappe

Arsenal pia wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, kuziba nafasi ya Alexis Sanchez ikiwa ataondoka. (Don Balon)

Thomas Lemar ameitaka klabu yake ya Monaco kumuuza kwenda Arsenal. (sun)

Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny anakaribia kuhamia Juventus kwa pauni milioni 8. (Daily Mirror)

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 29. (Star)

Chelsea wapo tayari kumpa mkataba wa miaka mitano winga wa Atletico Madrid Yannick Carasco, 23. (Don Balon)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka Toni Kroos, 27, kuwa sehemu ya mkataba wowote utakaomhusisha David de Gea kwenda Real Madrid. (Sun)

Kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Real Madrid, Toni Kroos

Manchester United wanaonekana kukaribia kumpata kiungo wa Inter Milan Ivan Perisic. (Daily Mirror)

Zlatan Ibrahimovic amekataa nafasi ya kujiunga na LA Galaxy na anapanga kusaini mkataba mpya na Manchester United. (The Sun)
Paris Saint-Germain wanapanga kutoa euro milioni 150 kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio. (Don Balon)
AC Milan wananamnyatia mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24. (Gazzetta dello Sport)

Barcelona wapo tayari kutoa euro milioni 65 pamoja na Ivan Rakitic ili kumsajili Marco Verratti kutoka PSG. Calciomercato)

Mchezaji wa Paris Saint-Germain, Marco Verratti  

Tottenham wanataka kujaribu tena kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. Timu hizo mbili zimeshindwa kukubaliana ada ya uhamisho ya mchezaji huyo. (Independent)

Tottenham wana matumaini ya kukamilisha usajili wa beki wa Estudiantes, Juan Foyth, 19, mwishoni mwa wiki hii. (Mirror)
Loic Remy, 30, anatazamiwa kuondoka Chelsea msimu huu, huku Everton na Southampton zikimtaka. (Metro)

West Ham watapanda dau la tatu kumtaka winga wa Stoke Marco Arnautovic, 28, baada ya dau la awali kukataliwa. (Sky Sports)

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents