Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Mshambuliaji wa Timu ya taifa ya Brazili na klabu ya  Barcelona, Neymar mwenye umri wa miaka 25, amewaambia wachezaji wenzake, Lionel Messi na Luis Suarez, kuwa atabakia Barca baada ya wawili hao kumshawishi kutojiunga na Paris Saint-Germain kwa uhamisho utakaovunja rekodi ya dunia wa pauni milioni 200. (Sport)

Mshambuliaji wa Timu ya taifa ya Brazili na klabu ya  Barcelona, Neymar

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemtaka Neymar kutohamia PSG na kusubiri kwenda Manchester United wakati utakapowadia. (Diario Gol)

Meneja wa Inter Milan, Luciano Spalletti ameionya Manchester United kwa kusema watoe pauni milioni 48 kama wanamtaka Ivan Perisic, vinginevyo wasahau kumsajili winga huyo. (The Sun)

Tokeo la picha la Inter milan player Ivan Perisic

Mchezaji, Ivan Perisic

Arsene Wenger amedai kuwa PSG wanataka kumsajili Neymar kwa sababu wameshindwa kumsajili Alexis Sanchez. (Daily Mirror)

Monaco wamesema wanataka pauni milioni 55 kumuuza winga Thomas Lemar mwenye umri wamiaka 21, ambaye anasakwa na Arsenal. (Daily Star)

Tokeo la picha la Monaco player,Thomas Lemar

Winga wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar

Manchester United wapo tayari kuwapa PSG pauni milioni 70 ili kumsajili kiungo, Marco Verratti. (Daily Express)

Marco Verratti amesema chaguo lake la kwanza ni kwenda Barcelona, ingawa pia yuko tayari kwenda Manchester United. (Express)

Manchester United wapo tayari kupanda dau kwa kipa chipukizi wa Bolton Wanderers Jake Turner mwenye umri wa mikaka 18. (The Sun)

Juventus wameacha kumfuatilia kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic mwenye umri wa miaka 28 na hivyo kutoa mwanya kwa Manchester United kukamilisha uhamisho wake. Chelsea wamesema wanataka pauni milioni 40 ambazo Juve hawapo tayari kutoa. (Telegraph)

Tokeo la picha la Chelsea, Nemanja Matic

 

Kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ametoa “hakikisho la 100%” kwa mashabiki kuwa kipa David de Gea atakuwepo Old Trafford msimu huu mpya. (Telegraph)

Manchester United na Arsenal huenda wakapambana kumsajili winga wa Real Madrid, Marco Asensio mwenye umri wa miaka 21. (Don Balon)

Klabu ya Deportivo la Coruna wamempa mkataba wa miaka kumi, Lucas Perez katika jitihada za kumshawishi mshambuliaji huyo wa Arsenal kurejea katika timu yake  hiyo ya zamani. (DXT Campeon)

Tokeo la picha la Arsenal strikere, Lucas Perez

Mshambuliaji wa Arsenal, Lucas Perez 

Mazungumzo ya uhamisho wa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 28 kwenda PSG yameporomoka kutokana na bei kubwa ya ada ya uhamisho na mshahara anaodai. (Le Parisien)

Arsenal wanajiandaa kupanda dau la takriban euro milioni 30 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho. (Record)

Chelsea wataongeza bidii katika kutaka kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23, wiki hii ingawa huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City. (Express)

Chelsea wanataka kuwazidi kete Manchester United na AC Milan katika kumsajili mshambuliaji wa Fluminese Ricjardlison. (Gianluca Di Marzio)

Jurgen Klopp amesema kiungo wake Emre Can haendi popote. (Liverpool Echo)

Liverpool wanasubiri kuona kama Southampton watakuwa tayari kuzungumzia uhamisho wa Virgil van Dujk. (Liverpool Echo)

Tokeo la picha la Liverpool need sign Virgil van Dujk

Mchezaji,Virgil van Dujk

West Brom wanajiandaa kutoa pauni milioni 10 kumsajili beki wa Manchester United Chris Smalling, 27. (Daily Star)

Matumaini ya Liverpool kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita yamefifia baada ya klabu hiyo kusisitiza kuwa haumuuzi mchezaji huyo. (Sky Sports)

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents