Michezo

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Mancheter  City wanajaribu kuwapiku mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya klabu ya  Real Madrid katika kumsajili mshambuliaji, Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 18, kutoka Monaco. (Daily Mirror)

Mshambuliaji, Kylian Mbappe

Manchester City wapo tayari kutoa pauni milioni 160 kumsajili Kylian Mbappe katika harakati za Pep Guardiola kujenga kikosi chake. (ESPN)

Kylian Mbappe ambaye alipachika mabao 15 katika mechi 29 za ligi ya Ufaransa ( Ligue 1) msimu uliopita anahitaji kujiunga na Real Madrid. (Daily Star)

Manchester City hawajapanda dau lolote zaidi ya pauni milioni 160, ingawa Pep Guardiola amesema Real Madrid hawana ‘msuli’ mkubwa wa kifedha kama wa City. (Sky Sports)

Real Madrid wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili Kylian Mbappe kwa Euro milioni 180 sawa na pauni milioni 161 (Marca)

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho anakaribia kujiunga na Barcelona (Mundo Deportivo)

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho

Barcelona wametuma maafisa wake nchini Uingereza kujaribu kumsajili Coutinho mwenye umri wa miaka 25, licha ya Liverpool kukataa dau la pauni milioni 72. (Sports)

Liverpool wanasisitiza kuwa Philippe Coutinho hauzwi, lakini Barcelona wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 80. (Daily Star)

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema timu yake haiogopi ‘kumwaga fedha’ msimu huu huku wakiendelea kumsaka beki wa Southampton, Virgil van Dijk, 26. (Daily Mirror)

Liverpool wanatarajiwa kukamilisha usajili wa Virgil van Dijk kutoka Southampton ifikapo mwisho wa dirisha la usajili. (Sky Sports)

Arsenal hatimaye wanakaribia kumsajili kiungo wa Monaco, Thomas Lemar mwenye umri wa miaka 21, kwa pauni milioni 45. (Sun)

Kiungo wa Monaco, Thomas Lemar

Arsenal wanafikiria kumsajili kiungo wa Nice, Jean Michael Seri. (L’Equipe)

Arsenal wanakabiliwa kupata hasara kwa mshambuliaji wake Lucas Perez, baada ya Deportivo La Coruna kutoa pauni milioni 9 kutaka kumsajili mchezaji huyo, 28. (Evening Standard)

Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere mwenye umri wa miaka 25, anataka kubakia London iwapo ataondoka Emirates, huku West Ham ikionekana ni kimbilio lake. (Independent)

Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere

Stoke City wanataka kununua wachezaji kadhaa katika wiki chache zijazo, lakini hawana mpango wa kumtaka winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Stoke Sentinel)

Kiungo wa Bayern Munich, Renato Sanches, 19, amesema anataka kuondoka Ujerumani huku AC Milan na Manchester United wakimnyatia mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 43. (Independent)

Kiungo wa Bayern Munich, Renato Sanches

Tottenham wanafikiria kumsajili beki wa Hoffenheim Jeremy Toljan, 22, baada ya mazungumzo ya kumsajili beki Ricardo Pereira, 23, wa Porto kukwama. (Daily Mail)

Everton wamepanda dau la pili la pauni milioni 45 kutaka kumsajili kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson. (The Telegraph)

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents