Michezo

USAJILI: Usajili wa Javier Hernandez waweka rekodi West Ham

Klabu ya West Ham United inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imethibitisha kumsaini mshambuliaji wa Bayer Leverkuden, Javier Hernandez ‘Chicharito’ kwa dau la pauni milioni 16.

Javier Hernandez akisaini miaka mitatu katika klabu ya West Ham

Javier Hernandez mwenye umri wa mika 29 aliwasili jijini London siku ya Jumatatu kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya afya  ili kutimiza uhamisho wake wa mkataba wa miaka mitatu kukitumikia kikosi cha West Ham.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Sky sport kinaeleza kuwa mshambuliaji huyo atakuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya klabu hiyo na anatarajiwa kulipwa pauni 140,000 kwa wiki.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Mexco, Hernandez amesema kuwa anafurahi kupata nafasi ya kujiunga na klabu hiyo.

“Ninafurahia kujiunga na West Ham United, kwangu mimi Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) ni ligi bora zaidi duniani na hivyo kupata nafasi kama hii siwezi kuiacha.

“Haya kuwa maamuzi magumu sana kwangu kuamua kurudi Uingereza. West Ham ni klabu yenye historia kubwa na inamalengo makubwa ndiyomaana hata usajili wake kipindi hiki cha majira ya joto umekuwa mzuri.

“Nimekuwa na kipindi kizuri cha miaka mitatu nikiwa nchini Hispania na Ujerumani lakini Uingereza inasalia kuwa mahala pangu sahihi katika kurasa zangu za maisha na jaskia furaha kuona nimerejea tena.

‘Chicharito’, amewahi kuichezea klabu ya Manchester United kwa misimu minne kati ya mwaka 2010 na 2015, na kufanikiwa kushinda magoli 59 kati ya michezo 156 aliyocheza kabla ya kujiunga na Real Madrid msimu wa mwaka 2014/15.

Hernandez ametumia misimu minne Manchester United, na kufanikiwa kushinda mataji mawili ya Premier League

Mpaka sasa West Ham imefanikiwa kuwasajili wachezaji, Javier Hernandez ‘Chicharito’ Joe Hart Pablo Zabaleta Marko Arnautovic katika dirisha hili la usajili.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents