Habari

Usajili wa vitambulisho vya taifa kwa watumishi wa umma waongezewa muda

Serikali imekubali kuongeza muda wa usajili wa watumishi wa umma katika vitambulisho vya taifa NIDA kwa wiki mbili ili kutoa nafasi kwa watu ambao hawajasijiliwa kupata fursa ya kufanya hivyo.

nchemba1

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba amesema baada ya muda huo kuisha, zoezi hilo litaendelea kwa wananchi wengine.

“Kutokana na changamoto zilizojitokeza katika zoezi la usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa, tumepokea maombi ya kuongeza muda wa usajili katika halmashauri mbalimbali. Tumeyatafakari na tumekubaliana na tumeafikiana kwamba tutaongeza muda huo wa usajili na utoaji wa vitambulisho kwa wiki mbili ili kutoa fursa kwa watumishi wa umma ambao hawajasajiliwa,” alisema Nchemba.

“Hivyo waajiri wote ambao watumishi wao hawajasajiliwa katika zoezi hili naomba watoe ushirikiano kwa maafisa wanaoendesha zoezi hili ili kuhakikisha zoezi hili linakamilika katika muda huo tulioutaja.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents