Michezo

USAJILI: Yanga wajiandae – Pius Buswita (Video)

Mchezaji mpya wa klabu ya Yanga SC kiungo, Pius Buswita amesema ametimiza malengo yake aliyojiwekea ya kuzichezea moja kati ya klabu kubwa hapa Tanzania hii ni baada ya mchezaji huyo aliyekuwa akikipiga katika kikosi cha Mbao FC msimu uliomalizika kuingia kandarasi na wana Jangwani hao.

Mchezaji mpya wa klabu ya Yanga SC kiungo, Pius Buswita wakwanza(kushoto)

“Najisikia furaha kwa sababu ni moja kati ya malengo yangu ambayo nilikuwa nimejiwekea kujiunga na moja kati ya timu kubwa hapa Tanzania”.

“Katika kikosi cha Yanga ningependa kuvaa jezi namba tatu kwa sababu ni ‘Dedication’ ambayo nilikuwa nimeshawekewa kutoka kwa Wazazi wangu”.

“Napenda kuwaambia mashabiki wa Yanga wajiandae nimekuja kuwaletea furaha na kuwaonyesha kile nilicho nacho na uwezo nilio nao naamini watafurahi sana, ilikuweza kuongeza mataji na kufanya vizuri kimataifa”.

“Kwa mashabiki wa Mbao FC, nashukuru kwa sapoti yao ambayo wamenionyesha na kuniamini”. Pius Buswita ameyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa klabu ya Yanga SC.

https://www.instagram.com/p/BVZ9YGmh6gA/?taken-by=yangasc

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents