Michezo

USAJILI: Yanga wananita ‘mtoa roho’ – Okwi (+Video)

Baada ya kuingia mkataba na klabu ya Simba SC, mchezaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi amewashukuru Watanzania kwa kumuonyesha upendo na kuahidi kuisaidia timu hiyo kutwaa mataji katika mashindano yanayowakabili.

Mchezaji Emmanuel Arnold Okwi (katikati) akiingia mkataba na viongozi wa Simba SC

Alipoulizwa kwanini wanamuita mtoa roho Okwi amesema ni kwa sababu ya kuwafunga Yanga,.

“Watanzania wamenionyesha mapenzi makubwa sana na watu wake ni wakarimu sana, najiskia raha sana nikiwa Tanzania na nawapenda kama wanavyonipenda.

“Mtoa roho kwa sababu ni ya kuwafunga Yanga tukiwa tunacheza nao, nakumbuka sana muunganiko wetu tulipokuwa na Mafisango,Felix Sunzu pamoja na Haruna Moshi ‘Boban’ ilikuwa kila tukiingia uwanjani tunafanya vizuri.

“Nashukuru sana kiongozi wangu wa Simba kwa kunikaribisha tena siku yaleo kujiunga na timu yangu, ni mekuja hapa kufanya kazi na viongozi ambao wananjaa sana ya kupata mafiniko kwenye msimu ujao.

“Nimekuja kupambana na kuhakikisha tunachukua ubingwa na kupambana katika mashindano ya kimataifa, namshukuru sana bosi Mohammed Dewji kwa kufanikisha huu usajili wa mimi kurejea tena Simba SC. Emmanuel Okwi ameyasema hayo kupitia mtandao wa klabu hiyo.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents