Habari

Usalama waimarishwa katika majengo ya bunge Ujerumani

Gazeti la Ujerumani la Bild limeripoti kuwa polisi imeimarisha usalama katika majengo ya bunge ya Ujerumani mjini Berlin kufuatia uvamizi uliotokea katika majengo ya bunge nchini Marekani.

Protesters and police outside the Reichstag

Gazeti hilo limenukuu barua ya Rais wa Bunge la Ujerumani Wolfgang Schaeuble kwa wabunge nchini humo. Schaeuble ametaka ripoti kutoka ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani juu ya ghasia zilizotokea katika majengo ya bunge nchini Marekani na kuwa serikali itatoa maelekeo zaidi na mafunzo watakayoyapata katika uvamizi wa Marekani ili kulilinda bunge.

Mnamo siku ya Alhamisi, msemaji wa polisi alisema watachukua hatua zaidi ili kuimarisha usalama katika majengo muhimu mjini Berlin, akiashiria jengo la Reichstag lenye makao ya bunge ya Ujerumani na sehemu zenye mafungamano na Marekani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents