Michezo

Ushahidi wa ex, wamweka pabaya Oscar Pistorius, asema alimsaliti na Reeva Steenkamp

Mpenzi wa zamani wa Oscar Pistorius jana alitoa ushahidi mahakamani mjini Pretoria kuwa mwanariadha huyo anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi wake kuwa aliwahi kupiga risasi juu ya paa la gari wakiwa na kwamba alimcheat na mwanamke (Reeva Steenkamp)
aliyemuua mwaka jana.

Oscar Pistorius in court
Oscar akiwa mahakamani

Msichana huyo aitwaye, Samantha Taylor, aliyelia mara mbili wakati akitoa ushahidi, alisema Pistorius alikuwa akibeba silaha mara zote wakati walipokua wapenzi na wakati mwingi alikuwa akimkakalipia yeye na marafiki zake. Kulikuwa na minong’ono mahakamani humo baada Taylor kudai uhusiano wao uliisha baada ya Pistorius kumcheat na Reeva Steenkamp.

Oscar Pistorius-1710867.png

Taylor alisema uhusiano wake na Pistorius ulianza mwaka 2011 alipokuwa na miaka 17 na uliisha November 2012. Alisimulia miongoni mwa tabia za Pistorius ni pamoja na kulala na silaha karibu na kitanda chake. Alisimua jinsi Pistorius alivyowahi kupiga risasi juu baada ya polisi kuwasimamisha kutokana na kuendesha gari kwa kasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents