Michezo

Ushahidi wa kesi ya Aveva, Kaburu haujakamilika

Kesi inayowakabili rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ imekhairishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kutarajiwa kusikilizwa tena Septemba 18 mwaka huu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa Mashtaka kuwa wakweli katika upelelezi wa kesi inayomkabili, Evans Aveva na Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa baada ya Wakili wa Serikali, Nassor Katuga kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na wangali wanasubiri nyaraka kutoka kwa mtaalamu wa maneno.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa akautaka upande wa mashtaka kuwa wakweli na kuhakikisha upelelezi ukamilika na ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18, 2017.

Picha za viongozi wa Simba SC, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents