Habari

Ushahidi wa tukio la Lissu utakusanywa hapa Tanzania – Jaji Mkuu

Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Juma amesema kuwa tukio la Mhe. Lissu la kupigwa risasi na watu wasio julikana ni uhalifu sio mdogo huku akisema kuwa ushahidi wa tukio hilo utakusanya hapa hapa Tanzania.

Jaji Mkuu, ameyazungumza hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa asikudanganye mtu kuwa mtu atatoka nje kuja kukusanya ushahidi huo.

“Tukio la Lissu ni la kihalifu nadhani tumekubaliana uhalifu mkubwa, sio mdogo ni jaribio la kuua lakini kitu cha kwanza ni kukusanya ushahidi na huo ushahidi utakusanywa hapa hapa Tanzania, asikudanganye mtu kwamba mtu atatoka nje atakusanya ndio atakuwa na uwezo wa kukusanya ushahidi , ushahidi tunakusanya hapahapa,” amesema Jaji Mkuu Juma.

Hata hivyo Jaji Mkuu amesema kuwa wao kama Mahakamani kanuni zao haziwaruhusu kutoa maoni au kuongelea jambo ambalo wanaliona moja kwa moja linaenda mahakamani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents