Burudani

Ushahidi wadai Drake alimshambulia Chris Brown


Mwanamuziki wa R&B Chris Brown amezungumza na polisi wa jijini New York, NYPD, kuhusiana na ugomvi uliotokea kwenye bar na uliomsababishia jereha kwenye kidevu.
Mtandao wa TMZ umeambiwa kuwa mwanasheria wake ameipa NYPD “ushahidi wa macho” unaodai kuwa rapper Drake alihusika kwenye varangati hilo.
Mtandao huo umesema umeambiwa kuwa mwanasheria wa Chris, Mark Geragos,ameenda jana NYPD kukabidhi ushahidi unaoonesha kuwwa Drake na Meek Mill walimshambulia.
Hata hivyo awali, Chris aliongea na polisi hao mahali kusikojulikana mjini New York, ambapo polisi waliuambia mtanda wa TMZ kuwa Chris sio mtuhumiwa bali ni shahidi na muathiriki wa ugovi huo.
TMZ umesema umeambiwa kuwa kwa sasa Drakesi mtuhimiwa pia.
Pia umedai kuwa Drake amekuwa akishirikiana na polisi japo haujui kama ni yeye ndiye aliyeongea nao japo inaonesha kuwa wawakilishi wake ndio waliozungumza na polisi.
Vyanzo vimeuambia mtandao huo kuwa mchokozi hapa ni Chris na kambi yake ambaye alikuwa akimsumbua Drake na watu wake usiki mzima wa jana.
Ripoti zingine zimedai kuwa mwanamke raia wa Australian alijeruhiwa usoni kutokana na ugomvi huo wa Chris Brown na Drake.
Msichana huyo mwenye miaka 24 ajulikanaye kwa jina la Hollie C, alikuwa kwenye klabu ya usiku ya SoHo ambapo alipigwa na chupa usoni.
Imedaiwa kuwa Hollie ameshonwa nyuzi 16 upande wa kulia wa kichwa chake.
Wapambe wa Drake na Chris Brown, ambaye aliwahi kumpiga mpenzi wake Rihanna, wamekanusha kuanzisha ugomvi huo.
Chanzo cha ugomvi huo ni chuki kati yao iliyotokana na uhusiano mfupi kati ya Drake na Rihanna baada ya kuachana na Chris Brown.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents