Bongo MovieMahojianoVideos

Ushauri kutoka kwa Jini Kabula kwa wanaotaka kuingia katika uigizaji [Video]

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=eja8OtlEcPo[/youtube] Msanii wa maigizo Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye amepata umaarufu mkubwa, lakini hataki kukurupuka kuivamia filamu sababu ya kuogopa kutumiwa vibaya. Mwigizaji huyo ambaye alitamba na kujizolea umaarufu kwenye filamu ya Jumba la Dhahabu, alisema wasanii wengi wamekuwa wakiwatumia wasanii wenzao kwa maslahi yao na kuwalipa kiasi kidogo cha fedha.

Alisema yeye ataendelea kuwepo katika kundi la Tuesday Kihangala Film, kwakuwa mkataba wake unalipa vizuri kulingana na tamthilia moja moja, kama Red Apple na Milosis. Anasema akiwa kwenye Tamthilia mkataba wake unambana kufanya kazi nje ya kazi hiyo.

Jini Kabula aliendela kusema sanaa ni uwito na amewashauri wanaotaka kuingia katika sanaa ya uigizaji kwamba wasijiingize kwa sababu maalum kama kuuza sura, fashion ama kujitafutia wanaume na wanawake. Wasanii wanatakiwa wajiheshimu kwa sababu wao ni kioo cha jamii.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents