Moto Hauzimwi

Ushindani wa Diamond na Alikiba ni mzuri ila…! – Lamar

Producer Lamar kutoka studio za Fish Crab amesema ushindani wa Diamond na Alikiba ni mzuri ila unapovuka mipaka na kutoka nje ya muziki siyo kitu kizuri.

Lamar na Diamond

Hata hivyo Lamar ambaye ameshafanya kazi na wasanii wote wawili amesema yeye kama producer hawezi kuwa na upande (team) ambayo anaishabikia.

“Ushindani wao mzuri kwa sababu unaleta changamoto kwetu kama arts na producer tuweze kufikia level zao, kwa ushindani wao ni mzuri ila pale wanapokuwa wanatoka nje ya mipaka na maadili yetu ndio wanakuwa wanakosea lakini ushindani wao wa kibiashara ni mzuri sana,” Lamar ameiambia Bongo5.

“Hayo mambo ya team ni mashabiki, siwezi kusema nampenda tu Diamod au Alikiba, no!, ni watu ambao nimekuwa nao nimewafanyia kazi, kwa hiyo mimi kama producer siwezi kuwa nasapoti team” ameongeza.

Katika hatua nyingine amezungumzia nyimbo walizotoa hivi karibuni wasanii wao ‘Seduce Me na Zilipendwa’ ambazo zilikuwa na ushindani mkubwa hasa mtandaoni.

“Nyimbo zote nzuri kila mmoja ana ladha yake ambayo ameileta, hazifanani zipo tofauti, kwa hiyo kila mtu ame-play part yake vizuri” amesema.

Lamar ameshatengeneza hit ya Diamond ‘Moyo Wangu’ pamoja na ile ya Alikiba ‘My Everything’.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW