Soka saa 24!

Ushindi wa Mshechu kuja na baraka nyingine

images2
mwanamuzuziki toka Tanzania Peter Msechu, ameibuka kidedea kuwa mshindi wa pili katika shindano lililokuwa likiendeshwa Kenya, maarufu kama Tusker Project  All Star, ambalo lilikutanisha washiriki wa tamasha hilo ambao mwanzo walifanya vizuri lakini hawakufanikiwa kushinda, na kupata nuru mpya ya kutoa wimbo na Kidumu.

 

Shindano hilo la Tusker All Stars lililoanza June mwaka huu limefikia fainali 14 August mwaka huu kwa kuibua washindi hao watatu ambao ni Alpha Rwirangira toka Rwanda (TPF 3 – Winner),Peter Msechu toka Tanzania (Mshindi wa 2 – TPF 4) na Davis Ntare toka Uganda (TPF 4 – Winner) wameibuka washindi na wamepata shavu la kupiga show same stage na wasanii wa kimataifa baadaye mwaka huu nchini Kenya….

Washiriki wengine walikua Hemedi Suleiman toka Tanzania,Caroline Nabulime na Amileena Mwenesi toka Kenya,Bernard Ng’ang’a na Patricia Kihoro toka Kenya walishiriki na walikaa wiki 8 na Ma Mc walikua ni Prezentaz maarufu Eve D’Souza toka Kenya na Gaetano Kagwa toka Uganda na mbali na washindi hao 3 kupata shavu la ku-share stage moja na wasanii wa kimataifa,haijafunguliwa kama watapata zawadi au vp….!

Hata hivyo Msechu anasema hivi karibuni antarajia kuachia ngoma yake mpya itakayokwenda kwa jina la Relax, ambayo itaitolea albamu kwa nyimbo hiyo ambaypo ilimpa chati sana katika Tusker Project.

Pia amesema hivi sasa anasambaza matisheti yenye nembo hiyo, inayoitasngaza wimbo huo alioshirikiana na Kidumu. Mwisho alimalizia shukrani zake kwa watanzania wote waliompigia kura, na shukrani zake kwa Blog hii kwa kumpigia kampeni.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW