Habari

Usiku wa Khanga za Kale

 

Mbunifu mkongwe kutoka Faibak Fashion Asia Idaruos Hamsini  amezungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa  atafanya onyesho liendalo kwa jina la ’Usiku Kanga za kale 2010’.

Asia alisema kuwa onyesho hilo litafanyika  siku ya Ijumaa tarehe moja October katika Ukumbi wa Diamond Jubilee  ikiwa na lengo la  kukuza hadhi ya kanga , na kwasababu  kanga ni moja ya vazi la Mtanzania.

Awali  Asia aliongezea kuwa kutakuwepo na burudani kutoka Morden Taarabu ,Khadija Kopa,Rukia Ramadhani,Sabah Mchacho,na Baby Madaha kutoka BSS watakaotumbuiza na pia wabunifu wa mavazi na mastaa mbalimbali watapanda jukwaani kuonyesha mavazi ya kanga.

Onyesho hilo limedhaminiwa na Tusker Lager , Michuzi Blog,Big Solution, Antelope Tours, Clouds FM,Mlimani Television,Valye Spring,Mryard,Channel Ten,Habari Co-operation,TBC1, Full shangwe, Abaya Center, Gema Sound, I-View photography, Eventlights,pamoja na Shear illusion.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents