Uncategorized

Uso kwa uso na Chui akivuta bangi mafichoni, apiga simu polisi kuomba msaada (+picha)

Jamaa mmoja ambaye aliingia kwenye nyumba iliyotelekezwa nchini Marekani ili avaute bangi alipatwa na mshtuko asioutarajia.

Alikutana na Chui mkubwa aina ya Tiger ambaye alikuwa ametelekezwa.

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Shirika la habari la BBC, Polisi jijini Houston, Texas wamesema awali bwana huyo alipowapigia simu walidhani kuwa yupo kwenye njozi (baada ya kuvuta bangi).

Lakini walipofika walimkuta Tiger mkubwa amefungiwa ndani ya kizimba.

Houston Police Department's Major Offenders, Livestock Animal Cruelty Unit arrived at scene and found a 350-pound tiger inside

Hakukuwa na alama yeyote iliyoonesha kuwa kuna watu waliokuwa wkiishi kwenye jengo hilo, japo kulikuwa na nyama mbichi karibu na kizimba hicho.

Polisi sasa wanasema watafanya uchunguzi ili kubaini namna gani mnyama huyo alifika hapo.

The home was abandoned but several packages of meat were found with the animal

Wameeleza kuwa “raia mwema” ambaye aligundua uwepo wa tiger huyo hakuwa akiishi kwenye nyumba hiyo, na aliingia tu ili “avute bangi”.

“Tuliwauliza iwapo kama wamelewa dawa za kulevya (bangi) ama kweli wamemuona tiger,” msemaji wa polisi amewaambia wanahabari.

Polisi pia wameeleza kuwa kizimba hicho hakikuwa madhubuti, na kilikuwa kimefungwa na bisbisi na kamba ya plastiki.

The cage that kept the animal enclosed was not large or sturdy enough for such a creature of that size so it had to be taken away

Japo mnyama huyo hakuwa mwenye hasira, ilibidi kwanza apigwe dawa ya usingizi kabla ya kumtoa kwenye nyumba hiyo na kupelekwa kwenye maskani ya wanyama.

The man told police he thought he was hallucinating when he first saw the overweight female tiger in the property's garage (Pictured, BARC's Animal Enforcement Officers with the animal)

Tigers ni aina ya Chui wanaopatikana Kusini na Kusini Mashariki mwa Asia na mashariki ya mbali ya Urusi. Ni wanyama ambao wapo katika hatari ya kupotea. Inakadiriwa kuwa wamebaki 4,000 tu mwituni.

The animal will be taken to an animal shelter temporarily before being moved to a permanent home

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents