Technology

Utafiti: Kuchat online kunaathiri mazungumzo asilia ya uso kwa uso

Internet imerahisisha mawasiliano kwa kiasi kikubwa kwa watu kuchat duniani kote lakini profesa mmoja anadai kuongezeka kwa mawasiliano ya mtandaoni kanaweza kuwa na madhara katika maisha halisi ya binadamu.

IMG_7372

Professor Sherry Turkle, wa Massachusetts Institute of Technology, anaamini kuwa uhusiano wa kwenye mtandao huwafanya watu wawe na urahisi wa kumpuuzia yeyote au kitu chochote wanachohisi kinaboa au kutoa majibu yaliyopangwa zaidi.

Professor huyo anaonya kuwa pale watu wanapoongea uso kwa uso kwenye maisha ya kawaida hujikuta wakihangaika na kujikuta wakisahau jinsi ya kuzungumza ana kwa ana. Anadai kuwa teknolojia inatishia kutawala maisha yetu, kutufanya tujitenge zaidi na kupingukiwa ubinadamu.

Anadai kuwa teknolojia inatuondoa kutoka kwenye mawasiliano ya binadamu halisi kwenda kwenye yale ya kimtandao ambayo yanageza ulimwengu halisi. Aliongeza kuwa mitandao ya kijamii inaweza kutufanya tuwe kama vichaa.

Anasema tabia hii inaweza kuwa kubwa zaidi kwakuwa watoto wengi wanatumia internet na simu wakiwa na umri mdogo.

Professor Turkle ni mwandishi wa kitabu kiitwacho: Alone Together: Why We Expect More from Technology and Less from Each Other, and The Second Self. Professor huyo alisema matumizi ya mitandao ya kijamii ni namna ya ‘wehu wa kisasa’ (modern madness).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents