Habari

Utafiti: Mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha ongezeko la uhalifu duniani

Utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa mabadiliko ta tabia nchini yana uhusiano mkubwa na ongezeko la vitendo vya kikatili duniani.

climate-change

Wanasayansi wa Marekani wamebaini kuwa hata mabadiliko kidogo ya joto ama mvua huchochea ongezeko la mashambulizi, ubakaji, mauaji pamoja na vita. Timu hiyo imesema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuwa makubwa, dunia inaelekea kuwa sehemu katili zaidi.

Utafiti huo umefanywa na chuo kikuu cha California, Berkeley.

Watafiti hao wameangalia tafiti zingine 60 duniani kote ambapo data zimekusanywa kwa mamia ya miaka.Mfano ni
pamoja na ongezeko na ukatili wa majumbani nchini India wakati wa kipindi cha ukame hivi karibuni na ongezeko la mashambulizi, ubakaji na mauaji wakati wa joto nchini Marekani.

Ripoti hiyo imedai kuwa ongezeko la joto lina uhusiano na migogoro ikiwemo vita vya wenyewe barani Afrika. Hata hivyo wamedai kuwa kuna uhusiano wa kisaikolojia pia kwasababu tafiti zingine zinaonesha kuwa joto huwafanya watu wawe rahisi kupata hasira.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents