Afya

Utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Srbonne Paris Cite, wataja vinywaji hivi vya sukari vinavyosababisha Saratani,fahamu zaidi

Utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Srbonne Paris Cite, wataja vinywaji hivi vya sukari vinavyosababisha Saratani,fahamu zaidi

Vinywaji vya sukari ikwemo maji ya matunda vinaweza kuongeza hatari ya saratani , kulingana na mwanasayansi wa Ufaransa. Uhusiano huo ulifichuliwa na utafiti uliochapishwa katika jarida la matibabu nchini Uingereza , uliwachunguza watu 100,000 kwa kipindi cha miaka mitano.

Kwa mujibu wa BBC. Wanasayansi hao kutoka chuo kikuiu cha Srbonne Paris Cite wanadai kwamba ongezeko la viwango vya sukari katika damu huenda ndio sababu kuu.

Hatahaivyo utafiti huo haukupata ushahidi kamili na kwamba watafiti wametaka utafiti zaidi kufanywa.

Je ni nini kinachohesabika kama kinywaji cha sukari?

Watafiti wao walisema kwamba ni kinywaji kilicho na zaidi ya asilimia 5 ya sukari. Vinywaji hivyo vinashirikisha maji ya matunda ambayo hayajongezwa sukari,

Vinywaji visivyo na pombe, vinywaji vya kuongeza nguvu, chai na kahawa yenye sukari.

Kundi hilo pia lilichunguza vinywaji visivyo na kalori vinywaji vilivyo na sukari yake lakini hawakubaini uhusiano wowote na saratani.

Je hatari ya saratani ni ya kiwango gani?

Utafiti huo pia ulifichua kwamba unywaji wa mililita 100 za ziada za vinywaji vilivyo na sukari kwa siku ikiwa ni chupa mbili kwa wiki kutaongeza hatari ya saratani kwa asilimia 18. Kwa kila watu 100 katika utafiti huo kuna 22 walio na saratani.

Hivyobasi iwapo wote watakunywa mililita 100 kwa siku itasababisha aina nyengine nne za saratani – na kuongeza jumla hiyo kufikia 26 kwa 1000 katika kipindi cha miaka mitano, kulingana na watafiti.

Kati ya visa 2,193 vilivyopatikana wakati wa utafiti huo aina yaaratani 693 zilikuwa zile za matiti , 291 zilikuwa za tezi dume na visa 166 vilikuwa vile vya saratani ya mwisho wa utumbo.

Kunywa kinywaji chenye sukariHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Je hili ndio thibitisho kamili?

Hapana – jinsi utafiti huyo ulivyofanyika inamaanisha unaweza kupata mifano katika data lakini hauwezi kuelezea.

Hivyobasi ulionyesha watu waliokunywa sana takriban mililita 185 kwa siku walikuwa na visa vingi vya saratani ikilinganishwa na wale waliokunywa chini ya mililita 30 kwa siku.

Na maelezo yanasema kuwa vinywaji vya sukari vinasababisha saratani.

Lakini pia watu wanaobugia vinywaji vya sukari wanaweza kuwa na matatizo mengine ya kiafya.

Hivyobasi utafiti huo hauwezi kusema kwamba vinywaji vya sukari ndio chanzo cha saratani.

Aliongezea kwamba kupuguza kiwango cha sukari katika chakula chetu ni muhimu sana.

Huku utafiti huo ukishindwa kutoa ushahidi kamili kuhusu sukari na saratani, inaonyesha mpango uliopo wa kupunguza kiwango cha sukari , alisema Dkt Amelia Lake kutoka chuo kikuu cha Teesside.

Je tatizo hilo linahusishwa na kunenepa kupitia kiasi?

Kunenepa kupita kiasi ni sababu moja inayosababisha saratani na matumizi ya juu ya vinywaji vya sukari husababisha mtu kunenepa.

Hatahivyo utafiti huo ulisema sio visa vyote.

Kunenepa kupitia kiasi kunako sababishwa na kunywa vinywaji vingi vya sukari uhusishwa lakini hawakuelezea uhusiano wote kwa kina, Dkt Mathilde Touvier mmoja wa watafiti hao alliambia BBC News.

Mchoro huu unaonyesha mwili wa mwanamke na viungo vya mwili ambapo kunenepa kupoitia kiasi husababishwa.

Je watengenezaji wa vinywaji vya sukari wanasemaje?

Muungano wa watengenezaji vinywaji visivyo na pombe nchini Uingereza wanasema kuwa utafiti huo hautoi ushahidi.

Mkurugenzi mkuu Gavin Prtington aliongezera: Vinywaji vyetu ni viko salama na ni miongoni mwa vya lishe bora.

Sekta ya utengezaji wa vinywaji hivi ina jukumu katika kusaidia kukabiliana na kunenepa kupitia kiasi na ndio sababu tumepunguza kiwango cha sukari na kalori.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents