Habari

Utafiti: Wanafunzi wa chuo kikuu huangalia simu mara 11 katika kila kipindi darasani

Kuongezeka kwa matumizi ya simu (smartphones) kwa vijana, kunaweza kuwa na athari ya moja kwa moja katika mafanikio yao wakiwa wakubwa.

social-networks-masthead.20131010231035

Utafiti uliofanywa kwenye chuo kikuu cha Nebraska-Lincoln umebaini kuwa mwanafunzi wa chuo wa kawaida huangalia simu yake mara 11 katika kila kipindi, na zaidi ya asilimia 80 wanaamini kuwa simu zinaingilia muda wao wa kujifunza.

Zaidi ya nusu ya wanafunzi kwenye majimbo matano ya Marekani waliwaambia watafiti wa chuo kikuu hicho kuwa huangalia jumbe za simu na kutembelea mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter sababu masomo yanaboa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents