Habari

Utafiti: Wanasayansi wa Marekani wadai kugundua chanjo ya kuangamiza virusi vya Ukimwi

Wanasayansi nchini Marekani wamedai kugundua chanjo ambayo wanaamini itaweza kuangamiza kabisa Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa binadamu.

chanjo

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika mtandao wa BBC, wanasayansi hao wameelezea kuwa chanjo hiyo imefanyiwa majaribio kwa nyani na kufanikiwa kuangamiza virusi wanaofanana na VVU waitwao SIV, na sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.

Taarifa za kisayansi zinaonesha kwamba Simian Immunodeficiency Virus (SIV) ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga ya maradhi kwa nyani, na vimekuwa vikienea kwa njia ya kujamiiana miongoni mwa vizazi vya nyani.
Wanasayansi hao wamesema kati ya nyani 16 waliopewa chanjo hiyo waliyoipa jina la Cytomegalovirus (CMV),tisa walipona kabisa maradhi ya SIV. Taarifa hiyo imeongeza kuwa kwa kawaida nyani ambaye ameambukizwa SIV hufa ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Mtaalamu wa Taasisi ya Chanjo katika Chuo Kikuu cha Oregoni ambaye alihusika kwenye utafiti huo, Profesa Louis Picker aliielezea chanjo hiyo kuwa ni ya kutia moyo ukilinganisha na nyingine ambazo zimewahi kufanyika.

Picha: Mtandaoni

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents