Habari

UTAFITI : Wanawake waongoza kwa maambukizi ya Ukimwi

Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu amesema kuwa Watanzania wapatao milioni 1.4 wanaishi na Virusi vya Ukimwi ambapo utafiti unaonyesha watu wazima wenye umri wa miaka 15 hadi 64 yako juu kwa wanawake kwa asilimia 6.5 ikilinganishwa na asilimia 3.5 ya wanaume.

Matokeo hayo yamewekwa wazi leo wakati wa uzinduzi wa viashiria na matokeo ya Ukimwi Tanzania kwa mwaka 2016/017 ambayo yamezinduliwa na Makamu wa Rais, Mama Samia.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu(NBS), Dkt Albina Chuwa amesema kwa mara ya kwanza utafiti huo ulifanyika mwaka 2003/04 ambapo kiwango cha maambukizi ya Ukimwi kilikuwa kwa asilimia 7.0

Hata hivyo kazi ya utafiti huo ilianza mwezi Oktoba 2016 mpaka mwezi Agosti mwaka huu ambapo jumla ya Kaya 14,811 zilishiriki kikamilifu kwenye mahojiano na utoaji wa damu na kufanya kiwango cha mwitikio kuwa zaidi ya asilimia 94.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents