Habari

Utafiti: Wanywaji wa kahawa kuishi miaka mingi zaidi

Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika na kuhusisha watu takribani 500,000 kutoka nchi 10 za Ulaya na kuchapishwa katika jarida na Annals of Internal Medicine, umebaini unywaji wa kahawa kwa vikombe vitatu kwa siku kunaweza kukusababishia kuishi miaka mingi zaidi.

Hata hivyo wataalamau hao wanasema ni vigumu kubaini moja kwa moja kuwa unywaji kahawa unachangia watu kuishi miaka mingi au ni maisha ya kiafya wanayoishi wanywaji.

Watafiti kutoka shirika la Agency for Research on Cancer and Imperial College London, wanasema wamegundua kuwa unywaji wa kahawa nyingi unahusiana na hatari kidogo ya kufariki hasa kutokana na magonjwa ya moyo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuchunguza takwimu kutoka kwa watu wenye  umri wa zaidi ya miaka 35, watafiti walitaka kujua kuhusu kiwango cha kahawa walichokuwa wakinywa na kutazama idadi ya vifo vilivyotokea miaka 16 iliyopita.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents