Fahamu

Utafiti waonyesha mtandao wa Instagram, umekuwa Chanzo cha gharama za harusi duniani, fahamu zaidi

Utafiti waonyesha mtandao wa Instagram, umekuwa Chanzo cha gharama za harusi duniani, fahamu zaidi

Mipango ya harusi katika kizazi hiki inawezekana kuwa sio rahisi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Utafiti uliofanyika nchini Uingereza unaonyesha namna ambavyo mitandao ya kijamii inavyochukua nafasi kubwa katika maandalizi ya harusi.

Gharama ya kuandaa harusi imeongezeka kwa wastani wa paundi thelathini na mbili elfu, kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2019.

Wapenzi wengi huwa wanatumia mitandao ya kijamii kama P interest na Instagram kuandaa siku yao kubwa ya harusi.

Hii inapelekea gharama ya harusi uwa kubwa zaidi kwa sababu karibu maharusi wote wanataka kuonekana vizuri kwenye Instagram.

Hannah kisses her fiance while showing her engagement ring to the cameraStylist Hannah Muller alitangaza kumchumbia mpenzi wake kupitia mtandao wa kijamii

Hannah Muller,mwenye umri wa miaka 20, anayetoka Afrika Kusini anapanga harusi yake kufanyikia London na anaisifu Pinterest kuwa msaada mkubwa kwake.

Bride leaves her ceremony with the train of her dress covered in coloured confetti

“Nimeweza kupata ukumbi mzuri sana mtandaoni,”alisema.

“Pinterest imekuwa rafiki yangu wa karibu wakati wa kuandaa harusi yangu. Ninaweza kufanya kila kitu na kupata kila kitu ninachokifikiria mtandaoni.”

Asilimia 42 ya wapenzi wanasema kuwa wanapata msukumo mkubwa kuwa na ndoa ya mitandao ya kijamii. kwa mujibu wa tafiti.

Na robo yao wanasema kuwa wako tayari kupanga bajeti yao ili harusi zao zipendeze kama za Insta.

Hannah alitangaza uchumba wake kwa kupiga picha inayoonyesha amevaa pete ili kuwajulisha marafiki zake kuwa amechumbiwa .Picha hiyo peke yake ilimgharimu paundi 200.

Na hii yote inatokana na shauku ya kujulisha watu katika instagram juu ya furaha yako.

Married couple being showered in confetti

Sandi Chahal ambaye ni mmiliki wa mapambo ya harusi na kuandaa sherehe anakiri utofauti uliopo.

“Kila mtu huwa anaongelea kuhusu ndoa aliyoiona Instagram, hivyo mitandao ya kijamii inamfanya kila mtu kuwa na shauku na mitandao ya kijamii jambo ambalo lilikuwa tofauti miaka 20 iliyopita”.

“Wateja wetu wanataka mapambo kwa ajili ya kupigia picha ambazo wataweka kwenye mitandao ya kijamii. Na wanataka waonekane sawa na wale waliowaona kwenye mitandao ya kijamii hicho ndicho wanakitaka maharusi wa sasa”.

Married couple walk down the aisle as colourful confetti is thrownHaki miliki ya pichaEVA PHOTOGRAPHY

Picha nzuri kwa ajili ya mitandao ya kijamii ndio jambo la pekee ambalo maharusi wengi wanataka.

Mitandao ya kijamii imeweka wazo la kutangaza harusi kuwa tukio ambalo watu wanapaswa kulifurahia na sio kulipa sura ya kuwa jambo gumu”.

Lauren (right) and her bridesmaidHaki miliki ya pichaJAMES GOURLEY PHOTOGRAPHY

Lauren Reynolds, 29, kutoka Hertfordshire, alikiri kutumia Pinterest kupanga harusi yake mwaka 2016.

A moodboard of a bride and groom's relationship with photos and notesHaki miliki ya pichaJAMES GOURLEY PHOTOGRAPHY

Mpiga picha Georgia Rachel, 24, kutoka Norfolk, anaamini kwamba harusi za sasa, maharusi wanapaswa kufurahia zaidi lakini wanapaswa kuwa makini na namna ambavyo watu wanapokea picha zao.

Namna ya upigaji picha wa harusi umebadilika na hata mitindo wanayovaa maharusi imebadilika.

“Kile ambacho kinawagawa maharusi wa sasa na wa miaka ya nyuma ni mitindo ya upigaji picha”

Hata kama idadi ya waalikwa inaweza kuwa ndogo , ila idadi ya picha zinazoweza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii inajumuisha walengwa wote ambao maharusi wanataka waone harusi yao.

Marries couple pose for wedding photo with pink smoke bombs in the backgroundHaki miliki ya pichaGEORGIA RACHEL

“Maharusi wanataka picha abazo zitawashangaza wengi mitandaoni.

Gharama ambazo zinatumika kuandaa muonekano mzuri wa picha za harusi instagram ndio zinawagharimu wapenzi wengi kutumia kiasi kikubwa cha fedha tofauti na kabla ya mitandao hiyo kuepo”.

Joanna and her fiance on a boatHaki miliki ya pichaRHYS SHEA
Image captionJoanna na mchuma wake

Maharusi huwa wanajali watu wangapi watapenda picha zao mitandaoni.

“Nimekuwa nawaza kuhusu picha kuanzia mwanzo wa maandalizi ya harusi kwa sababu picha zinachukua sehemu kubwa ya harusi” alisema Joanna May, kutoka London.

Joanna showing her engagement ring to the cameraHaki miliki ya pichaJOANNA MAY
Image caption

Joanna alitangaza uchumba wake Instagram

“Kwa ujumla, mitandao ya kijamii inasaidia sanawatu kuandaa harusi zao na kufanya zifane. Picha zinapokuwa nzuri ndio furaha kwetu”.

Chanzo BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents