Fahamu

Utafiti waonyesha uongo ndio kitu kinachoiunganisha jamii, Fahamu zaidi

Utafiti waonyesha uongo ndio kitu kinachoiunganisha jamii, Fahamu zaidi

Kwa binaadamu imegundulika kwamba uongo huenda ndio jambo linalotuunganisha pamoja kijamii. Na licha ya kwamba hawawezi kuficha uongo wanapofanyiwa ukaguzi kwa mashini ya kutambua uongo, huenda kuna mbinu ndogo inayoweza kutusaidia kuwatambua wasema uongo miongoni mwetu.

Mtaalamu wa masuala ya wanyama namhariri Lucy Cooke amefanya utafiti kubaiin kwanini uongo unadhihirika kwa wanyama na pia miongoni mwa binaadamu.

unaubadili ukweli ili kupata amani

Disloyal man walking with his girlfriend and looking amazed at another girlHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHuenda hutofaidika saa zote kwa kusema ukweli

Mara nyingi, tunachomaanisha tunaposema neno “uongo” ni kuwa mtu anapanga kuwadanganya watu kwa maneno au hatua zake. lakini mazungumzo ya kawaida yanaweza kufanyika tu kwasaabu hatusemi tunachokifikiria kwa uhalisi au tunachomaanisha.

Hebu k=fikiria iwapo katika kila mazungumzo unasema unachofikiria kwa kweli, je watu wangeweza kuvumilia?

Hata tusipopenda mtindo mpya wa mtu wa nywele, hatuwezi kuthubutu kusema hilo.

Tunatambua kwamba hakuna anayependa ukweli kwasababu huenda ukawana madhara kuliko faida na hili lipo kwa binaadamu wengi tu.

Kwahivyo, ni kweli uongo unatuunganisha pamoja, kuimarisha ushirikianoi na kuifanya dunia kuwana utulivu.

Thuluthi moja kati yetu hudanganya

A wooden Pinocchio figurine, sitting on a shelfHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSiwezi kusema uongo kamwe

“Karibu thuluthi moja kati yetu husema uongo kila siku,” anasema mwanasaikolojia Richard Wiseman.

Na utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa asilimia 5 ya idadi jumla ya watu duniani wanadai hawajawahi kusema uongo kamwe.

Inaonekana wengi wetu hawawezi kusema ukweli katika utafiti ambao watu hawakujitambulisha.

Ukitaka kujua mtu muongo, msikilize, usimtazame

Sababu kwanini hatuwezi kuwatambua waut waongo ni kwamba tumezoea kuangalia au kutazama.

Sehemu kubwa ya ubongo wetu unatumika kutazama na kwahivyo mara nyingi watuhutumia ishara hiyo wakati wakujaribu kubaini iwpao mtu anasema uongo.

Je wanahangaika walipokaa? wanatumia mikono, uso wao umekaaje?

Hatahivyo, baadhi ya vitu hivyo nimambo yanayoweza kudhibitiwa, waongo walioboboea wanatambua kwamba mtu anajaribu kuwangalia kuona iwapo wanadanganya.

Ishara kando na hayo inatokanana yanayosemwa, tunachosema na namna tunvyokisema.

Hili ni jambo gumu kwa waongo kulidhibiti – kwahivyo ukiliangazia hilo zaidi na unajua unachostahili kukitafuta unakuwa hodari wa kuwatambua waongo.

Watu waongo kwa jumla husema mambo machache, wao huchukua muda mrefu kujibu swali na huepnda kujitenga katika uongoa wanoasema, kwahivyo hawawezi kutumia maneno kama ‘mimi’, au ‘yangu’.

Dunia imejaa waongo

Close up of a surprised looking chickenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUsimuamini kuku

Uongo upo kila mahali. Duniani, wanyma hudanganyana kila saa kwa rangi au tabia ili kuendeleza vizazi vyao.

Chukua mfano wa ngisi anayejigueza kuwa mwanamke ili kumpita mwanamume, kwa kuficha umbo lake ubavuni mwake dhidi ya mpinzani wake.

Na usimuamini kuku… majimbi huwavutia kuku wa kike kwa kutoamlio kwamba kuna chakula. na wakati hakuna huwahadaa kujamiiana badala ya kula chakula.

Lakini wanasayansi wamejifunza kuwa hata ndege wanaojamiiana – hushiriki katika ujanja, mahusiano ya nje wanapofikiria wanaweza kuimarisha fursa yao ya kupata watoto bora wenye afya.

Historia ya kusema uongo ilianza wapi?

Three chimpanzees sitting on a rock, each looking in a different direction. Wildlife picture taken at Gombe, in Tanzania.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWakati ukweli unakuponza

Uongo ni muhimu katika kuweza kuishi katika jamii kubwa na tofuati duniani.

Kwa wanyama kama sokwe mtu, kuwa katika kikundi kuna manufaa yake , unaweza kugawanya jukumu la uwindajichakula na kuna macho ya ziada kujihadhari na wanyama hatari.

lakini unapokuwa kwenye ushindani na wengine kula chakula, inaweza kuchangia vita ambapo wewe au mwingine anaweza kujeruhiwa, na hilo huligharimu kundi zima.

Kwahivyo ina manufaa zaidi kwako kuwa mjanja kuliko kwa kundi zima.

Na tabia za uongo kwa manufaa ya kujikinga ina historia ndefu katika mageuzi ya viumbe katika jamii.

Línea

Kwahivyo pengine kusema uongo siojambo baya. maana bila ya kusema uongo, hatungekuwepo hapa leo , ni muhimu kwa uhai wetu.

Lakini pengine ndivyo atakavyosema mtu muongo, sio??

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents