Habari

Utafiti: Wapenzi kulala vitanda tofauti usiku husaidia kuimarisha mapenzi yao

Swala la kulala vitanda tofauti kwa wapenzi linaweza kuwa na tafsiri mbaya kwa wapendanao lakini utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa matokeo yake yana faida zaidi ya hasara katika mahusiano.

couples separate beds-1

Utafiti uliofanywa Ryerson University huko Toronto, Canada, umeonesha kuwa kati ya asilimia 30 na 40 ya wanandoa hulala vitanda tofauti usiku, na wataalamu wanasema kujitenga wakati wa kulala kunaweza kuwa na faida zaidi katika kusaidia kuimarisha uhusiano zaidi ya madhara yake.

Colleen Carney, mwandishi wa utafiti huo aliiambia CBS kuwa, wanandoa (couples) wanaolala pamoja huwa hawapati kiwango cha usingizi kinachotakiwa. Badala yake hua wanajikuta wanaamshana mara kwa mara kwa milio mbalimbali (mikoromo) na kujigeuza mara kwa mara.

couples separate beds-2

Aliendelea kusema kuwa wapenzi wanapaswa wafikirie juu ya kulala tofauti kwa faida ya kupata mapumziko bora ya usiku na kuboresha mahusiano.

Carney pia alizungumzia dhana iliyozoeleka kuwa wanandoa au wapenzi wakilala tofauti basi wanakuwa wamegombana kwa kusema kuwa ‘Watu wanaweza kuwa na uhusiano mzuri sana na wa kuridhisha kwa kulala mbali mbali, watu wengine wanaweza hata kuwa wanaelekea kupeana talaka lakini kwa kulala tofauti inaweza kusaidia wakarudisha mapenzi yao’.

Alitoa mfano wa wapenzi wa Canada walioishi kwa kulala vitanda tofauti kwa miaka 14 na mpaka sasa ni wanandoa wenye furaha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents