Habari

Utafiti: Watu wanaoongea lugha nyingi wana mvuto zaidi

Utafiti uliofanyika nchini Marekani na Uingereza umebaini kuwa watu wanaozungumza lugha nyingi wana mvuto zaidi.

160823130417-tourist-international-flags-exlarge-169

71% ya Wamarekani na 61% ya Waingereza, wanaamini kuwa kuongea lugha zaidi ya moja kunamfanya mtu awe na mvuto.

Katika watu 3,000 wanaozungumza Kiingereza waliofanyiwa utafiti Marekani na Uingereza, 9 kati 10, walikiri kujifunza lugha mpya katika msako wa mapenzi.Karibu nusu yao walisema wana ndoto ya kuwa na uhusiano na mtu wa nchi nyingine.

Pia mmoja kati ya wanne katika utafiti huo anaamini kuwa kujua lugha moja kumewakwamisha kitaaluma. Pia mmoja kati ya nane alikiri kuongeza chumvi kwenye CV kuhusu uwezo wa lugha zingine.

Kwa dunia nzima, zaidi ya nusu huweza kuzungumza zaidi ya lugha moja, lakini wazungumzaji wa Kiingereza nchi za magharibi wako nyuma sana.

Utafiti wa mwaka 2001 ulionesha kuwa ni robo tu ya Wamarekani wanaweza kuzungumza lugha ya pili, tena wengi ni Spanish, huku utafiti wa mwaka 2014 wa Eurobarometer ulionesha kuwa 60% ya watu wa UK na Ireland wanaongea lugha moja tu – Kiingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents