Burudani

Utajiri wa Beyonce na Jay Z ni shida!

By  | 

Couple ya Jay Z na Beyonce inazidi kujitengenezea heshima zaidi duniani.

Kwa mujibu wa Forbes wawili hao wanautajiri wa dola bilioni 1.16. Katika utajiri huo Jay kiasi chake ni dola milioni 850 na Queen Bey kiasi chake ni dola milioni 350.

Hivi karibuni, jarida hilo liliwataja ‘The Carters’ kushika namba mbili katika orodha ya Forbes Five. Wakati huo huo, rapper huyo anatajwa kuweza kushika namba moja kwa kuingiza mkwanja mrefu kwa mwakani kutokana na hivi karibuni kuongeza mkataba mpya wa miaka 10 ambao utamfanya kuingiza kiasi cha dola milioni 200 kupitia kampuni ya Live Nation ambayo itakuwa ikiandaa matamasha ya msanii huyo na kusimamia promotion.

Kwa mwaka jana jarida hilo liliwataja wawili hao kuwa ndio couple ya watu maarufu walioingiza fedha nyingi zaidi kwa kuweka benki dola milioni 107.5.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments