HabariUncategorized

Utajiri wa Rais Donald Trump waporomoka

Jarida la Forbes leo limetangaza majina ya matajili 400 nchini Marekani na kwenye orodha hiyo imeonesha utajiri wa Rais wa Marekani, Donald Trump kuporomoka kwa kiasi cha dola milioni $600 kutoka Dola bilioni $3.7 mwaka jana 2016 hadi dola bilioni $3.1 mwaka huu.

Moja ya majengo ya kifahari ya kibiashara yanayomilikiwa na Rais Trump.

 

Kutokana na kuporomoka kwa ukwasi huo Rais Trump ameshushwa kutoka nafasi ya 156 mwaka jana hadi nafasi ya 248 mwaka huu.

Jarida la Forbes limesema kuporomoka kwa uchumi wake kumetokana na kushuka kwa soko la biashara ya ardhi (Real Estate) kama Nyumba, Hoteli, Appartments n.k jijini New York na gharama kubwa alizotumia kwenye kampeni za kugombea urais mwaka 2016.

Hii ndio orodha kamili ya matajiri 10 walioongoza kwenye orodha ya matajiri 400 wenye utajiri mkubwa nchini Marekani kwa mwaka 2017 .

1-Bill Gates kwa utajiri wa dola bilioni $89.

2-Jeff Benzos mmiliki wa amazon.com dola bilioni $81.9.

3-Warren Buffet dola bilioni $78.

4-Mark Zuckerberg mmiliki wa Facebook dola bilioni $71.

5-Larry Ellison mmiliki wa kampuni ya Oracle inayojihusisha na utengenezaji wa Software, anamiliki dola bilioni $59.

6- Charles Koch mmiliki wa makampuni ya Koch ana dola bilioni $48.5 .

7-David Koch huyu ni mdogo wake na Charles Koch nae anamiliki dola bilioni $48.5 .

8-Michael Bloomberg muanzilishi na mmiliki wa kampuni Bloomberg LP inayojihusisha na utoaji wa taarifa na takwimu mbalimbali za biashara na uchumi duniani. amekadiliwa kuwa na dola bilioni $46.8 .

9-Larry Page, ni mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya Google anamiliki dola bilioni $44.1 .

10-Sergey Brin, Mmiliki wa kampuni ya Alphabet Inc kampuni mama inayofanya kazi na Google, anamiliki dola bilioni $43.4 .

Chanzo: Jarida la Forbes .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents