Habari

Utakula mkate wa unga wa Senene? Wanafunzi wa Canada kuzalisha unga unaotokana na wadudu hao kulisha nchi maskini

Katika kukabiliana na tatizo la njaa hususan kwenye nchi maskini, wanafunzi wa Montreal, Canada wamegundua chakula cha uhakika.. unga uliotengenezwa kutumia senene au panzi na wadudu wengine waliwao.

article-2439974-186DAD0600000578-631_634x418

Ukipewa jina ‘Flour Power’, timu kutoka chuo kikuu cha McGill inapanga kuanza kuvuna senene kutoka kwenye nchi kama Mexico, Thailand na Kenya na kuufanya kutumika kutengeneza mikate na chakula kingine.

Zaidi ya tano 10 za senene/panzi zinatarajiwa kusafirishwa kutoka Mexico March 2014 na kundi hilo linapanga kuongeza aina ya wadudu watakaotumika kwenye mradi huo siku za mbeleni.

Senene hao watazalisha chakula cha uhakika lakini pia kuwawezesha wafugaji kupata kipato… Bukoba mpo?

Hult_Clinton
Wanafunzi hao wakikabidhiwa tuzo yao na Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton.

Proposal yao imeshinda tuzo ya mwaka huu ya Hult Prize na wanafunzi hao watano wamepokea dola milioni 1 kuigeuza kuwa kweli. Project hiyo ya Flour Power ilitengenezwa na wanafunzi wa MBA, Mohammed Ashour, Shobhita Soor, Jesse Pearlstein, Zev Thompson na Gabe Mott ambao kwa pamoja wanajiita Aspire Food Group.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents