Habari

Utapeli kwa kutumia simu za mkononi waendelea kudhibitiwa

Matapeli wanaojitambulisha kama wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kwa makosa ya kudukua taarifa za wateja wa huduma ya kifedha ya Tigo Pesa inayotolewa na kampuni hiyo ambapo wamekuwa wakiwatapeli wateja wa kampuni ya Tigo kwa kujitambulisha kama wafanyakazi halali wa Tigo wakati kiukweli sio waajiriwa wa Tigo.

Matapeli hao utumia mbinu hiyo kujipatia taarifa za siri za wateja hao ambazo baadae wamezitumia kuiba kiasi cha fedha zipatazo shilingi milioni 26 kutoka kwa wateja mbalimbali wa mtandao huo kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Hawa watu wana mbinu mbalimbali, tukitolea mfano, kuna ambao watakupigia wakisema aidha wamekutumia hela kimakosa, au anakupigia kutoka makao makuu ya kampuni ya simu husika na angependa utatue tatizo ambalo mteja amelalamikia.

Tulipata nafasi ya kumuhoji wakala mmoja, kwa jina la Amos Chirwa kutoka Kijichi, ambae alisema, ” kwa kweli matapeli ni wengi, na kila siku wanabuni njia tofauti tofauti ili waweze kutuibia sisi mawakala au wateja.

“Mimi kama wakala, ambae nina uzoefu wa miaka 6 sasa, ningependa kuwashauri watanzania kwa ujumla, kwamba usimpe mtu namba yako ya siri, au taarifa binafsi hata kama amejitambulisha kama mfanyakazi wa kampuni za simu kama Vodacom, Airtel, Tigo au Zantel”. Alimalizia kwa kusema.

Mtandao huu ungependa pia kuwaasa watanzania kutojishirikisha na masuala ya kiuhalifu hususan katika masuala ya simu za mkononi kwani serikali ina mkono mrefu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents