Utata MOI

MSAJILI wa Baraza la Madaktari Tanzania, Pilot Luwena, amewaandikia ilani ya kutoa maelezo madaktari saba wanaotuhumiwa kuhusika na upasuaji tata katika Taasisi ya Mifupa na Tiba Muhimbili (MOI).

na Lucy Ngowi

 

 

 

MSAJILI wa Baraza la Madaktari Tanzania, Pilot Luwena, amewaandikia ilani ya kutoa maelezo madaktari saba wanaotuhumiwa kuhusika na upasuaji tata katika Taasisi ya Mifupa na Tiba Muhimbili (MOI).

 

Ofisa Uhusiano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Victor Nyalali, alisema kuwa madaktari hao wametakiwa kujieleza kuhusu malalamiko hayo ndani ya wiki mbili tangu walipopokea barua.

 

Kwa mujibu wa Nyalali, hadi kufikia jana madaktari hao hawakuwa wamejibu ilani hiyo.

 

“Ni kweli msajili amepokea barua kutoka MOI, hivyo amewaandikia barua madaktari saba wanaotuhumiwa kwa sakata hilo wajieleze. Wamepewa wiki mbili,” alisema Nyalali.

 

Upasuaji huo tata umefanyika Novemba mosi, mwaka jana, katika taasisi ya MOI, baada ya wagonjwa wawili – Emmanuel Didas na marehemu Emmanuel Mgaya – walipofanyiwa upasuaji tofauti na magonjwa yao.

 

Kutokana na upasuaji huo tata, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, aliagiza bodi ya MOI iwafikishe mara moja kwenye Baraza la Madaktari wale madaktari wanaotuhumiwa kuhusika na sakata hilo.

 

 

 

 

 

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents